ZIFAHAMU FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita.
Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.

Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha afya cha Maryland nchini Marekani (University of Maryland Medical Center), Kitunguu swaumu kina viinilishe ambavyo hudhibiti bakteria (anti-bacterial), fangasi (anti-fungal ), virusi (anti-viral) na vijidudu nyemelezi (anti-parasitic) sifa inazokifanya kiwe na uwezo wa kutibu ugonjwa wa matatizo mbalimbali katika ngozi.

FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU.

Kitunguu swaumu kinao uwezo wa kuzuia usipate upele,mabaka mabaka na maambukizi mbalimbali katika ngozi na kukuacha na ngozi yako ya thamani ya asili na yenye kupendeza, hutibu mba kichwani, huondoa chunusi,miwasho katika ngozi na sehemu za siri na pia huondoa fangasi katika ngozi, Bawasiri ya nje,pumu ya ngozi.

Mikunjo na alama za kuzeeka mapema katika ngozi, Na maambukizi mbalimbali katika ngozi

Ili kujitibu matatizo mbalimbali ya ngozi tumia kitunguu swaumu kwenye kila chakula unachopika, kitumie kibichi katika maji au mtindi na pia pakaa mafuta ya kitunguu swaumu kila siku katika ngozi yako.

Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;

Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.

Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bakteria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.

Harufu ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.

Chanzo: Dr Fadhil Paul

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.