WATAWA,WANAKIJIJI WATAKIWA KUTUMIA BUSARA KUMALIZA MGOGORO WA ARDHI .

Na.Amiri kilagalila.

Wakazi wa Kijiji cha MADOBOLE Kata ya LUPONDE Wilayani NJOMBE pamoja na Shirika la Watawa wa Kanisa Katoliki wa Jimbo la Njombe Wametakiwa kutumia busara kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya Miaka Kumi na Tatu Sasa.

Kauli Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka mara baada ya kutembelea eneo lenye mgogoro na kusikiliza pande hizo mbili zinazogombewa eneo lililopo ndani ya eneo linalodaiwa kumilikiwa kisheria na watawa hao.

“Tutawatuma wataalamu hapa wachukue ramani ya shamba hilo lote namba 535 waje wapitie mipaka vizuri na waniambie watu wako sehemu gani,alafu tuje tukae tuone tunatokaje nia yangu nikuona ni lazima tunamaliza mgogoro huu kwa misingi ya kufuata sheria lakini pia kwa kujenga mahusiano kati ya waliopewa eneo, na wananchi waliokuwa wanajipatia ridhiki katika eneo hili ili kila mmoja awe huru kufanya shughuli yake”alizungumza Olesendeka.

Mara baada ya kumaliza kukagua eneo hilo OLE SENDEKA amezungumza na wananchi, viongozi wa siasa pamoja na watawa ili kusikiliza malalamiko yao ambapo bado kumeonekana na shida katika kuumaliza mgogoro huo.

“Lile shamba lipo kwenye milima yaani huwezi kusema utalima au kufanya kitu chochote ni shamba tu hata walioenda kupima wakasema haiwezekani na mbadala wa kipande hiki sisi watawa tulipewa na halmashauri na pana GPS kabisa kilichokuwa kikisubiriwa ni barua tu kufika wizarani”alisema mmoja wa watawa.

Kutokana na Hali Hiyo Mkuu wa Mkoa wa Njombe alitoa uamuzi wa kuitisha kikao cha pamoja ofisini kwake kati ya pande hizo zilizo kwenye mgogoro ili kujadili kwa kina na kumaliza mgogoro huo.

Wakati wa Ziara ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi Mkoani Njombe Alimuagiza Mkuu wa Mkoa Kufanya Ziara ya Kwenda Kutatua Mgogoro Huo Jambo Ambalo Limeanza Kutekelezwa.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.