WAJASIRIAMALI WA BURUNDI  WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUTATUA KERO MPAKA WA KABANGA

 

Na. Dinna Maningo,Bariadi.

Wajasiliamali kutoka Bujumbura nchini Burundi wameiomba Serikali ya Tanzania kutatua kero katika mpaka wa Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera ambao umekuwa kero pindi wanapoingia nchini na bidhaa zao  kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya Viwanda Vidogo SIDO.

Wakizungumza na mtandao wa Dar mpya kwenye maonyesho ya viwanda vidogo SIDO yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu ilielezwa kuwa maonyesho hayo yana jenga uhusiano wa kibiashara katika nchi hizo mbili.

Minani Floribert ambaye ni mwana sanaa mchongaji wa vinyago alisema kuwa licha ya kupewa barua za kushiriki katika maonyesho nchini Tanzania lakini wamekuwa wakisumbuliwa katika mpaka wa Kabanga na hivyo kujikuta wakilala siku 2 mpakani hapo bila kuruhusiwa kuingia nchini.

“Unakuta Nchi imetualika kushiriki maonyesho lakini tukifika mpaka wa Kabanga tunazungushwa sana licha yakuwa na vibari hii ilishatokea mara mbili mwaka 2017 tulizuiliwa tukalala siku tatu mpakani tulikuwa tunaenda kwenye maonyesho ya sabasaba -Dar es Salaam ukiwaambia wanakuzungusha kwanza  baadae ndo mnaruhusiwa.alisema.

Aliongeza” Mwaka huohuo tulialikwa maonyesho  viwanja vya mnazi mmoja tulizuiliwa mpakani siku mbili ya tatu ndiyo tukaruhusiwa tunaiomba Serikali ya Tanzania itusaidie nimefanya kazi hii kwa miaka 15 nazunguka Nchi mbalimbali kwenye maonyesho na kutoa Elimu kama nchi ya Tanzania,China,Senegal,Rwanda,Japan,Mali,Uganda,Kenya,Congo,Malawi na Kenya.alisema Floribert.

Fransine Nizigirimana anayajihusisha na ususi wa vikapu na mikeka alisema kuwa kupitia maonyesho hayo utangaza na kutoa elimu juu ya bidhaa zao wanazozitengeneza lakini pia maonyesho yakiisha ununua bidhaa za Tanzania na kwenda kuzitangaza Burundi.

“Naipongeza Tanzania kwani kupitia maonyesho ya SIDO tunapata fursa ya kutangaza bidhaa zetu kama hapa ninauza chombo kinachotumika kuweka ugali ili usipoe tunaita (Inkoko)kina tunza joto  kuliko ukiweka kwenye sahani baada ya muda ugali unakuwa na maji.alisema.

“Tukiondoka tunanunua bidhaa za Tanzania mf.ukinunua Batiki ya 12,000 Burundi tunauza 25,000 ,gauni (Dela)  tunanunua 6,000 unauza 15,000 lengo letu la kuleta biashara nikutaka kufahamiana  na kujenga mahusiano na Watanzania tujue  kazi zao na wao wajue kazi zetu pamoja na kupata changamoto mpakani ila tukishafika kwenye maonyesho hatupati usumbufu wowote” alisema Nizigirimana.

Nibogora Msheli alisema kuwa kazi ya ususi wa vikapu na mikeka ameifanya kwa miaka 13 nakwamba ni mara yake ya 4 kushiriki maonyesho nchini Tanzania katika mikoa ya Dar es Salaam,Dodoma,Mwanza na Simiyu.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.