WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUNZA KUMBUKUMBU MIAMALA MALIPO YA KODI KWA MIAKA 5 MFULULIZO

Serikali imewashauri wafanyabiashara wote nchini kutunza kumbukumbu zao za miamala ya ulipaji kodi katika kipindi cha miaka mitano mfululizo kama sheria ya usimamizi kodi ya mwaka 2015 kifungu cha 35 kinavyoelekeza.

Ushauri huo umetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo aliyehoji iwapo serikali itapokea kumbukumbu ya namba ya malipo iwapo mfanyabiashara atapoteza taarifa za miala zilizopo katika simu.

“Walipa kodi wajitahidi kuwa na kumbukumbu kama kifungu cha 35 cha sheria usimamizi kodi ya 2015 inavyoelekeza,” amesema na kuongeza Dkt. Kijaji.

“Sheria hiyo inaelekeza kila mlipa kodi anatakiwa kutunza kumbukumbu za ulipaji wa miamala kwa muda wa miaka 5 mfululizo.”

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.