UMUHIMU WA ASALI KAMA DAWA YA MAFUA.

ASALI NI NINI?

Asali ni chakula kitamu katika hali kiowevu kinachotengenezwa na nyuki.

Nyuki hula mbelewele pamoja na maji matamu ndani ya maua na kuitoa tena katika mzinga wa nyuki kwa kuitunza kwenye sega. Ndani ya sega kiowevu huiva kuwa asali kamili.

Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee.

Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na mdalasini.

Aidha, uchunguzi wa kila wiki unaofanywa na jarida la World News kuhusu tiba unasema, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea,imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na
mdalasini katika kujenga afya bora

UMUHIMU WA ASALI

>Hutibu chunusi

Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo watafiti wanasema changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee.

>Hutibu Ngozi Kama umeumwa na mdudu.

Asali, wanasema inairudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu waharibifu kama dondora, washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

>Kukatika kwa nywele.

Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15.

>Kuponya miguu iliyopasuka.

Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa dakika 30 kisha safisha kwa sabuni na maji. Tatizo litakwisha kwenye kipindi cha wiki moja.

>Hutibu Maumivu ya jino.

Changanya asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.

>Hutibu ugonjwa wa Mafua.

Mafua huwakera na kuwanyima watu wengi raha unaweza kupungua na kupotea kabisa ikiwa utatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo.

>Huamsha tendo la ndoa

Asali na mdalasini huaminika pia kuamsha hamu ya tendo la ndoa endapo itatumiwa kwa kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Hii inaokoa ndoa nyingi sana

>Huondoa mchafuko wa tumbo.

Asali ikichanganywa na mdalasini husaidia kuondoa mchafuko wa tumbo usababishwa na gesi ama vidonda vya tupo pia pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji na kuyanywa.

>Hupunguza tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu.

Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku ni muhimu pia kiafya kwani hupunguza uwezekano wa kutokea kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu.
Matumizi ya mara kwa mara ya asali na mdalasini wakati wa kifungua kinywa husaidia kuzuia uwezekano wa kupata ugonjwa wa moyo pamoja na kuzuia mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu.

Pia husaidia kuimarika na kuongezeka kwa kinga ya mwili kutokana na asali kuwa na hazina kubwa ya virutubisho na madini.

Unywaji wa kila siku wa kikombe baridi cha chai iliyowekewa na asali na mdalasini huimarisha afya bora na madhubuti kwa mtumiaji.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.