Tundu Lissu atoa ujumbe mzito kuhusu afya yake

Kupitia ukurasa wake wa mtandao, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anapatiwa matibabu nchini Ubeligiji aliandika;
“Wapendwa wangu natumaini wote hamjambo asubuhi hii (angalau kwangu ni saa 12 kasoro ya asubuhi).

Nawaomba msamaha kwa kuwaweka roho juu jana halafu sikuonekana. Nilipata wageni na by the time nimemalizana nao muda ulishaenda sana. Naomba nianze kwa kuwapa briefing ya afya yangu.

Wengi wenu mtakuwa mmeona video clips nikifanya mazoezi ya kutembea. Clip hizo zinaonyesha naendelea vizuri na ni kweli.

Operesheni ya mwezi uliopita imepona, angalau kwenye muscles. Mfupa bado una kazi kubwa kidogo na utachukua muda kupona.

Licha ya maendeleo haya mazuri, bado kuna operesheni moja zaidi inahitajika. Madaktari wangu walipaswa kuniwekea metal frame ya kusapoti mfupa uliofanyiwa operesheni mwezi uliopita.

Hata hivyo, hiyo ilishindikana kwa sababu operesheni yenyewe ilichukua muda mrefu sana (masaa 7) na nilipoteza damu nyingi sana.

Huu mguu uliumizwa sana kwa risasi. Ulivunjwa sehemu mbili na mfupa wa juu ya goti uliharibiwa sana. Kazi ya kuurekebisha ni ngumu sana kwa sababu hiyo.

Hata hivyo, madaktari – wa Nairobi na wa hapa – wamefanya kazi kubwa kuhakikisha wanautibu vizuri mpaka sasa naweza kusimama na kutembea, hata kama ni kwa kuchechemea kwa magongo.

Sasa kazi ya kuweka metal frame inatakiwa kufanywa kesho asubuhi ili kukamilisha tiba ya mguu huo. Na kazi hiyo ni surgery vile vile kwa kuwa wanahitaji kuunga mfupa huo kwenye metal frame itakayoushikilia na kuupa support.

Hilo likifanyika nitaweza sasa kuweka uzito wa mwili kwenye mguu na eventually nitaweza kutembea bila magongo. Nitawatumia picha as soon as possible ili muweze kuona kazi mnayoichangia kwa upendo na ukarimu mkubwa.

Madaktari wangu wameniambia kwamba hiyo metal frame itakaa mguuni kati ya miezi sita hadi nane. Hata hivyo, haina maana kwamba nitakaa hospitalini kwa muda wote huo.

Aidha, haina maana kwamba sitaweza kufanya kazi yoyote ile katika kipindi hicho. Kwa kushauriana nao, pamoja na nyie ndugu, familia na jamaa zangu na viongozi wenzangu, tutaangalia mambo ninayoweza kuyafanya wakati nikiwa kwenye safari ya full recovery.

Sasa naomba nimalizie kwa kuwashukuru tena kwa upendo na ukarimu wenu mkubwa.

Safari bado ni ndefu, lakini sasa mwisho wake unaonekana more clearly. Tulikotoka ni mbali na ni giza zaidi. Tunakoelekea ni karibu na kuna nuru kubwa zaidi.

Tumesafiri pamoja na kupita kwenye bonde la uvuli wa mauti tukiwa pamoja. Sasa tufike kwenye kilele cha matazamio yetu tukiwa pamoja pia.

Nawashukuruni sana na Mungu wetu awabariki sana na awaongezee mlikopungukiwa”

Related posts

One Thought to “Tundu Lissu atoa ujumbe mzito kuhusu afya yake”

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.