TBA WAPONGEZA FAMARI STORE KWA KUWAPA MAFUNZO MAFUNDI RANGI IRINGA

WAKALA wa  majengo Tanzania (TBA )  mkoa wa  Iringa amepongeza  kampuni ya  Famari  Store  kwa  kutoa mafunzo kwa mafundi rangi  wa  mkoa wa Iringa na Njombe  kuwa  yatasaidia   kuongeza  ubora wa majengo mkoani hapa .

Menja  wa TBA  mkoa wa Iringa  Fazes  Tarimo ametoa  pongezi hizo jana  wakati  akifunga mafunzo ya   siku  moja  yaliyoandaliwa na kampuni ya Famari  Store  ya  mkoa  Iringa na  kuendeshwa  na  kampuni ya Slkcoat Print Co.Ltd  ya  nchini  Uturuki  kupitia tawi lake la  jijini Dar es Salaam .

Alisema kuwa  mafunzo hayo  ni mazuri ya  yanakwenda  sawa na mpango wa  serikali ya awamu ya  tano  chini ya  Rais Dkt  John Magufuli  kuelekea  uchumi wa  viwanda  na kuwa  kupitia mafunzo hayo  kutaongeza   ajira  kwa  vijana  na  kuwa na vijana wenye ujuzi  wa  matumizi  sahihi ya rangi .

Alisema  anatumaini  kuona  ubora  wa  upakaji wa rangi katika majengo  yanayoendelea  kujengwa  utazingatia  sifa   sahihi ya  upakaji wa  rangi   pia  kuwa na mafundi  wenye  utashi  wa  aina  za rangi  wanazotumia.

Mkurugenzi wa Famari  Store  ambao  ni  waandaaji  wa mafunzo hayo  Mohamed  Abri  alisema  kuwa  waqmekuwa na utaratibu wa  kutoa mafunzo  ya matumizi  sahihi ya  rangi  na  kuwa tayari  wametoa mafunzo kama  hayo ya  uchanganyaji wa rangi na upuliziaji  kwa  mafundi  magari  na  sasa  ilikuwa ni  zamu ya mafuni  rangi za  majumbani .

Abri alisema  kuwa mafunzo hayo  yametolewa kwa  mafundi  zaidi ya 100 kutoka  mkoa  wa Iringa na  mikoa ya  jirani  na kuwa   lengo  ni  kuwa na mafundi  wenye  uelewa  wa matumizi  ya  rangi .

Hivyo  alisema  wao kama  mawakala wa  rangi  kutoka kampuni ya Slikcoat  ya  nchini  Uturuki   wameona  ni vema  kuwapa mafunzo mafundi hao  ili  kusaidia   kurahizisha  uuzaji  wa rangi na kuwa na mafundi  wenye  uelewa wa kutosha  ambao watajua ni rangi aina gani  inapaswa  kupagwa  sehemu gani na namna ya  kuichanganya  na  kuipaka.

Aidha  alisema  kuwa  rangi    hizo  kutoka  nchini  Uturuki  zimekuwa zikihitajika  zaidi na  suala  ambalo  wao  wameliona ni  baadhi ya  mafundi   kutokuwa na uelewa wa  kuzitumia  lakini kwa mafunzo hayo  wanaamini mafundi hao  wataweza  kuwa  wabobezi wa upakaji  rangi .

Mkufunzi wa mafunzo hayo  kutoka kampuni ya  Slikcoat  Saleh  Ahmed  alisema  kuwa   mafundi hao  wameweza  kuonyesha  uelewa wa  kutosha baada ya  kufanyiwa majaribio  mara  baada ya mafunzo   hivyo  ni imani yake  kuwa na ubora  zaidi  katika kazi  yao .

Wakishukuru kwa  niaba ya washiriki  wengine wa mafunzo hayo  Iren Mathias  na  Jonas Mbasa   walisema  kuwa  kutolewa kwa mafunzo hayo  kutawaongezea  wateja  zaidi  na  kuwa badala ya  makampuni  kuchukua mafundi  rangi  kutoka   nje ya mkoa wa Iringa  sasa  watalazimika  kununua  rangi  Iringa na  kupata mafundi ndani ya  mkoa.

Mkurugenzi wa Famari Store Mohamed Abri akijadili jambo na meneja wa TBA mkoa wa Iringa Fezes Tarimo
Meneja wa Wakala wa majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Iringa Fezes Tarimo akimkabidhi mmoja kati ya washiriki wa mafunzo ya ufundi rangi Iren Mathias cheti ,mafunzo haya yaliandaliwa na kampuni ya Famari Store

 

Mkufunzi kutoka kampuni ya rangi za Slikcoat ya nchini Uturuki Saleh Ahmed akiwapa mafunzoya rangi mafundi rangi mkoani Iringa

 

 

 

 

 

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.