SPIKA WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI AMWANDIKIA BARUA SPIKA NDUGAI

Spika wa Bunge la Afrika la Mashariki-Eala,  Martin Ngoga amemuandikia barua Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akitoa pongezi kwa bunge hilo kwa maandalizi mazuri ya mkutano wa 4 uliofanyika kuanzia Aprili 8 hadi 27, 2018 katika ukumbi wa Msekwa ulioko bungeni jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa leo bungeni jijini Dodoma na Spika Ndugai wakati akitoa taarifa mbalimbali kwa wabunge.

“Spika wa Bunge ameniandikia barua kutoa shukrani za dhati kwa maandalizi mazuri yaliyopelekea mkutano kufanyika na kufanikiwa vizuri,” amesema Spika Ndugai.

Aidha, Spika Ndugai aliwashukuru wabunge na wadau wote kwa kushirikiana katika kufanikisha mkutano huo unaofanyika kwa mzunguko kila baada ya miaka 2 katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu ulifanyika hapa nchini.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.