SINGAPORE YASITISHA BIASHARA ZAKE NCHINI KOREA KASKAZINI

Nchi ya Singapore imesitisha shughuli zote za biashara na nchi ya Korea Kaskazini wakati ambapo Umoja wa Mataifa na Marekani wanataka kuiwekea vikwazo vikali nchi hiyo.

Forodha nchini Singapore zilisema kuwa, bidhaa za biashara kutoka Korea Kaskazini zilipigwa marufuku kuanzia tarehe 8 Novemba mwaka huu.

Imeelezwa kuwa, kwa wale watakaokiuka marufuku hiyo watafungwa kwa kipindi cha hadi miaka miwili.

Marufuku hiyo inachukuliwa baada ya Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini kufuatia jaribio ya sita ya bomu la nyuklia.

Singapore ilichukua nafasi ya nane kama mshirika wa kibiashara wa Korea Kaskazini. Ikumbukwe kuwa Rais Donald Trump wa Marekani, alishatoa onyo kali kwa Korea Kaskazini la kuwataka wasijaribu kuigusa nchi hiyo na badala yake ameitaka kukaa pamoja na kufanya mazungumzo..

Wakati hali hiyo ikiendelea kati ya nchi hizo mbili, raia wa Korea Kaskazini ameiomba Chinakuisaidia familia yake.
Asilimia kubwa ya biashara za korea kaskazini ni pamoja na China, mshirika mkubwa wa kiuchumi wa taifa hilo.

Awamu ya hivi karibu ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa ililenga makampuni na watu binafsi pamoja na makampuni mawili nchini Singapore.

Mwezi Januari mwaka 2016 kampuni moja nchini Singapore ilipigaw faini ya dola 125,000 kwa kusaidia kusafiridsha silaha kutoka nchini Cuba kwenda Korea Kaskazini baada ya mahakama kupata kuwa kampuni ya Chinpo wa usafiri wa baharini ilikiuka azimio la Umoja wa Mataifa.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.