RAIS WA UFARANSA AZUA MIJADALA BAADA YA KUMBUSU HADHARANI RAIS WA CROATIA

Rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarovic amezua mijadala mtandaoni baada ya kuonekana kwenye kamera akipigwa busu na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, hii ilikuwa wakati Ufaransa ilishinda Kombe la Dunia la 2018 juzi Jumapili Julai 15.

Bi. Kitarovic amezungumziwa sana ulimwengu mzima kwani amekuwa shabiki sugu wa michuano yote ya Kombe la Dunia ya mwaka huu, kwa sababu alionekana kila mara akiwatia moyo wachezaji wake, jambo lililowafurahisha wengi

Kolinda alisisimua mitandao ya kijamii hapo Jumapili siku ya fainali baada ya kuonekana kwenye kamera akipigwa busu na Rais mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron. Hii ilikuwa baada ya Ufaransa kushinda Kombe la Dunia la 2018 kwa kuicharaza Croatia mabao 4- 2 katika mechi ya fainali kule Urusi.

Rais huyo mrembo alionekana kuwa karibu na Rais Macron ambaye mwishowe walibusiana kutokana na furaha waliyokuwa nayo baada ya timu zao kufika fainali, na walionekana pamoja hadi wachezaji wote walipotuzwa moja baada ya mwingine.

Busu hilo liliwatatiza wengi kimawazo ikizingatiwa kuwa Macron amemuoa mwalimu Bridgette Macron ambaye wameishi naye kwa ndoa kwa miaka 10.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.