RAIS MAGUFULI AZINDUA CHUO CHA UONGOZI

Na Tatu Tambile

Raisi John Magufuli leo, Jumatatu amezindua Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika Wilaya Kibaha Mkoani Pwani kinachokusudiwa kulenga umoja uliokuwepo kati ya Watanzania na watu kutoka vyama vya ukombozi vya ANC, Frelimo, ZANUPF na vinginevyo barani Afrika.

Mhe. Rais Magufuli akipewa maelezo ya mwonekano wa chuo hicho utakavyokuwa mara baada ya ujenzi wake kukamilika

katika uzinduzi huo Rais Magufuli  alikitaka chuo kilete tija katika manufaa ya maendeleo ya kiuchumi kwa Waafrika wote na kuendeleza umoja.

‘’Chuo hiki kiwe dira kwa ajili ya Waafrika wote, chuo hiki kikalete ukombozi wa kweli na ukombozi wa sasa sio kupata  wa kupata Uhuru bali ni ukombozi wa maendeleo ya kweli ya kiuchumi’’. Alisema.

Baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi huo

Aidha Rais Magufuli alivishukuru vyama vyote ambavyo ni marafiki wa CCM vilivyoshiriki uzinduzi huo, ikiwemo Frelimo, ANC, Zanu-PF, SWAPO, MPLA kwa ushirikiano na kufanikisha suala hili na kuongeza kuwa anayoimani kuwa watumishi wake watakienzi chuo hiko.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.