RAIA WA KIGENI 129 WADAKWA WAKIOMBA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Raia wa kigeni takribani 129 wanashikiliwa mkoani Kigoma kwa kosa la kuingilia mchakato wa uandikishaji vitambulisho vya taifa.

Watu hao wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji wasio rasmi walikamatwa katika zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho ambapo walijitokeza kushiriki.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti alithibitisha taarifa hizo jana alipotembelea kituo cha Murusi ambapo walifika kujiandikisha ili wapate vitambulisho hivyo.

“Tumewashikilia watu hao kwa ushirikiano wa wananchi na maofisa uhamiaji. Niwaombe wale wote ambao si raia mjitokeze kabla hatujaanza kuwabaini,” alisema Jenerali Gaguti.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.