MBUNGE ATOA KALI YA MWAKA, ASHINDWA KUULIZA SWALI BUNGENI KISA MWEZI WA RAMADHANI

Mbunge Viti Maalumu anayewakilisha kundi la vijana bungeni, Khadija Nasiri Ali amesema ameshindwa kueleza masikitiko yake pamoja na kuuliza swali bungeni kwa sababu ya mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani.

Hadija ameyasema hayo leo katika kipindi cha maswali na majibu baada ya kutoridhishwa na majibu ya serikali kuhusu swali lake alilouliza namna mfuko wa vijana ulivyosaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

“Majibu yako kisera zaidi, kwa vile niko katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, nashindwa kueleza masikitiko yangu,” amesema Hadija.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde amesema mfuko wa vijana umewasaidia vijana kujikwamua kiuchumi ambapo hadi sasa vikundi vya vijana 397 wamepatiwa kiasi cha Sh. Bilioni 4 kwa ajili ya kuwawezesha vijana.

Waziri Mavunde amesema kuwa, serikali inaendelea kutekeleza mikakati yake kabambe ya kuwezesha vijana kiuchumi, ikiwemo kubadili mitazamo yao ya kutaka kuajiriwa baada ya kuhitimu elimu badala ya kujiajiri.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.