MAKALA:UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO MJINI WAKULIMA WAPANDA MBOGA KWENYE MIFUKO

Na Dinna Maningo,Mwanza.

Naianza safari hadi mtaa wa  Magaka Kata ya Kahama wilaya ya Ilemela km 16 kutoka Jijini Mwanza  Kaskazini Magharibi mwa nchini ya Tanzania ili kufahamu ni kwanini wakulima wameamua kupanda mboga ndani ya mifuko na kwenye vichuguu pamoja na kujua namna kilimo kinavyowasaidia katika kupunguza tatizo la uhaba wa mboga za majani.

Wanafunzi wa shule ya msingi Kahama wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wakimwagilia maji kichuguu walichokiandaa ili kupanda mboga za majani.

Nafika hadi shule ya msingi Kahama Kata ya Kahama  naona kundi la wanafunzi wakiwa wamevaa sare za shule  wasichana sketi ya rangi ya kijani shati nyeupe,Wavulana kaptura ya kaki na shati nyeupe wengine juu wakiwa wamevaa masweta na soksi nyeupe miguuni.

Nasogea hadi waliposimama wakiwa wameinama mkononi mwao wameshika  vidumu vilivyo na maji ndani yake  wakinyunyizia maji juu ya mboga za majani zilizopandwa juu ya vichuguu walivyovitengeneza na zingine zikiwa zimeota  ndani ya mifuko  ile inayohifadhiwa simenti baada ya kutumika .

Kwenye Kichuguu hicho zinaonekana mboga mbalimbali kama Chainizi,,Bamia,Pilipili Hoho,Mahindi Nyanya chungu na zingine zikiwa zimepandwa kwenye mifuko.

Mboga aina ya Chainizi ikiwa imeoteshwa ndani ya mfuko.

Erick Gunda mwanafunzi wa darasa la 5 shule hiyo anaeleza sababu ya wao kupanda kwenye mifuko na vichuguu,anasema kuwa mjini kuna uhaba wa maeneo ya kulima mashamba hivyo wameamua kupata mboga kwa njia hiyo ambayo haihitaji eneo kubwa la kilimo.

‘’ Maeneo ya vijijini kuna  baadhi ya mashamba yako wazi hayaendelezwi  kwa kilimo ikiwemo kilimo cha mboga za majani,huku watu waishio maeneo ya mjni wakitamani mashamba hayo yangekuwa mjini ili walime mboga za majani’’anasema .

Naom Mgeta Mwanafunzi wa darasa la 5 katika shule hiyo anasema kuwa Wanafunzi wa shule hiyo  wanalima bustani za mboga kwa kuzipanda kwenye mifuko na vichuguu ili kuboresha afya zao kwani zikishakomaa walimu wao uzichuma na kisha kuwapikia chakula wanafunzi na zingine kuwapelekea wazazi wao.

‘’Tunafundishwa na wataalamu wa kilimo akiwemo Salm Kapagala  upandaji huu umetusaidia tumepanda hadi majumbani kwetu badala ya kununua mboga tunachuma hizi tulizopanda maana kilimo hiki ni chepesi hakihitaji eneo kubwa na tumewafundisha wazazi wetu’’anasema Mgeta.

Levocuts Michael ni Mwalimu wa Mazingira shule ya Msingi Kahama anasema kuwa Wanafunzi ushirikishwa lengo kujfunza kilimo hicho  ambapo wameunda vikundi vya wanafunzi kwa kila darasa ujifunza na wao wanafundisha wenzao darasani na wakati wa umwagiliaji wanafunzi wengine utumia muda huo kujifunza na kuhoji maswali.

Salum Kapagala ni fundi sanifu Kilimo na Umwagiliaji Kata ya Kahama ambaye pia anatoa elimu ya kilimo cha mifuko na kwenye vichuguu ikiwemo shule ya Msingi Kahama anasema kuwa lengo ni kufikisha elimu kwa wananchi jinsi ya kutumia eneo dogo kupata mboga za majani,anaeleza jinsi yakuandaa kichuguu.

‘’Mahitaji ni Vigingi (Vijiti),mawe,tofali  kutengenezea shamba,majivu kwa ajili ya kuzua tindikali bacteria wasiharibu shamba,Kokoto,Nyasi Kavu,Kamba na mchanganyiko wa udongo na mbolea ya samadi  kisha tengeneza kichujio chenye kipenyo cha sm 30/sm 50 kulingana na ukubwa wa shamba lako.anasema

Kapagala anasema kuwa kwa wastani  shamba liwe na kipenyo cha  sm 300/3m ,kichujio huwa katikati ya shamba  na kinatengenezwa kwa vigingi virefu  1.0m, kama kinavyoonekana pichani, Kisha una sambaza majivu kote shambani na kwenye chujo  ili kuzuia bacteria wasiharibu kigingi kwa urahisi.

‘’  Kisha ambaza nyasi kavu kote  ili kutunza unyevunyevu,weka kokoto katika chujio mpaka juu kisha simamisha nyasi kavu ndani ya shamba  ili udongo usipotee ,kisha weka udongo ulo na uwiano katika shamba (udongo na samadi) mpaka shamba lijae  sambaza nyasi kavu .

Anazidi kueleza  kuwa baada ya hapo mwagilia maji yakutosha kupita chujio kwa muda wa siku tatu mfululizo mpaka kuwe na unyevunyevu wa kupanda kisha panda mbegu,au mche  kwenye shamba lako ,mwagilia maji kupitia chujio mara baada ya kupanda  na baada ya wiki mbili mboga uwa tayali kwa kuchumwa.

Maria Consosia ni mkulima wa mboga  za majani kwenye mifuko anaishi  mtaa wa Bulyanhulu Kata ya Shibula iliyoko wilayani Ilemela km 21 kutoka Mjini Mwanza anasema kuwa mboga hizo zinamsaidia hasumbuki kuzifata sokoni tena kwa gharama yeye uzichuma bure kwakuwa kazipanda nyumbani kwake eneo la wazi ambapo sokoni fungu moja uuzwa sh.500.

Emanuel Mabula mkazi wa Bulnhulu anajihusisha na kilimo cha umwagiliaji anasema kuwa ameanza kilimo hicho mwaka huu na alianza kwa majaribio kwa kuziotesha kwenye mifuko Kabeji,Bilinganya na Pilipili kujua kama zitaota na zimeota na matarajio yake ni kuwa na kipato kikubwa kitakachotokana na kilimo cha mifuko.

Afisa Kilimo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela  Neema Semwaiko anasema kuwa wanameamua ktuoa elimu ya kilimo kwa jia ya mifuko ili kuwajenga uwezo Wanafunzi wakue wakijua kilimo hicho lakini kiwawezesha kujitegemea.

Anaongeza kuwa halmashauri  hiyo ina jumla ya hekta 10,422 zinazofaa kwa kilimo lakini zinazolimwa ni 5,256,idadi ya wakulima  ni 25,000 na mazao yanayolimwa mahindi,Mtama,Mpunga,,Mihogo,Viazi vitamu,Maharage na Kunde,Pia kilimo cha Bustani kwa mboga na matunda  kamaMchicha,Chinese,Karoti,Bilinganya , matikiti maji,,Matango,Bamia,Nyanya chungu,Kabichi na Nyanya hoho.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.