MAGUFULI AENDELEA KUMMALIZA MBOWE, HAI DIWANI MMOJA ANG’OKA

Diwani wa kata Romu iliyopo Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Shilyimiaufoo mejiuzulu nafasi yake ya udiwani pamoja na kujivua uanachama wake wa Chadema na kujiunga chama cha Mapinduzi (CCM ).

Kimaro amechukua maamuzi hayo hii leo ambapo tayari amemwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hai kumtaarifu juu ya uamuzi wake huo.

Katika barua yake, Kimaro ametaja sababu kuu ya kujiuzulu udiwani na kujiunga CCM kuwa ni kukosekana kwa demokrasia ndani ya CHADEMA ambayo inaweza kuisaidia jamii katika kutatua matatizo na kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa Tanzania.

Kimaro amesema Chadema imekuwa ikipinga na kutokubali juhudi za maendeleo zinazoletwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Magufuli.

Aidha amesema, ameamua kujiunga CCM ili kuunga mkono juhudi za dhati zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.