KUNA HAJA YA MITIHANI YA TAIFA KUTOFAUTIANA KATI YA SHULE ZA MJINI NA VIJIJINI..

NA MWL.MGALA R.B

0715079380,0675967150
mgalaramadhan@gmail.com

Leo nimeona kwa kifupi sana kuwashirikisha sehemu ya tafiti zangu binafsi juu ya Elimu yetu,nikianza na Elimu ya msingi ikiwa ni utafiti nilio ufanya siku 180 kabla ya mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika tar 5&6 sep 2018.

Katika utafiti wangu niligundua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu zinafananafanana na zile zinazozikabili sekta zingine,Changamoto yeboyebo kama uhaba wa watumishi,Nyumba za walimu,Maslahi Zimetawala katika maeneo mengi ingawa juhudi za Serekali katika kuzitafutia ufumbuzi ni kubwa.

Ukiachiliambali changamoto hizo,Elimu katika sehemu za vijijini imegubikwa na Changamoto Mara dufu ukifananisha na zile za mijini mathalani kuna shule za mjini Zinaingia kwa Shifti Mchana na Asubuhi huku walimu wake wakifundisha kati ya vipindi 5-8 kwa wiki huku shule za vijijini walimu wake wakifundisha vipindi 25-40t kwa wiki.

Hatahivyo idadi ya wanafunzi katika darasa moja ni zaidi ya 90 huku shule za mjini ikiwa ni 40-50.hata na hivyo miundombinu kama majengo chakavu na ya zamani uhaba wa vyoo maji umeme hayo ni mambo yaliyozoeleka na sio matatizo tena kwa vijijini ni kama hali ya kawaida sasa ingawa kimsingi inaumiza.shule za mijini wao wana ahueni sana katika changamoto hiyo.

Maisha magumu sana ya familia za vijijini hii ni changamoto nyingine..Maisha magumu sana ya wazazi humfanya mtoto kuwa na mlundikano wa majukumu jambo linalomlazimu kuweka nyuma sana jukumu la msingi la kusoma.

Aidha kutokana na mpambano mkali sana wa maisha wazazi wa vijijini hawana mda kabisa wa kuwasihi watoto wao juu ya elimu na kuwasimamia hali inayolazimu jukumu hilo kuwa la walimu pekee.

Pamoja na uwepo wa sheria ndogondogo na mikakati ya kisera ambayo pengine inajaribu kuwasogeza wanajamii karibu na taasisi za elimu bado hali inashinikiza jamii kujitenga mbali sana na sekta za elimu.

Wanafunzi wa vijijini kupata motisha za kielimu na hata kuahidiwa mambo mazuri wakifanya vizuri kwenye mitihani ndio hadithi kabisa na simulizi wanazozisikia tu kwa watu hatahivyo vitabu vya ziada vinavyoweza kuwapa nyongeza ya maarifa pengine ni ndoto za mchana na hayo hayatokei kwao na walishazoea.

Pamoja na changamoto hizo na mazingira magumu sana bado wanafunzi wa vijijini watoto wa masikini kabisa wanaobaki shule kwa huruma tu za elimu bure bado wanajitahidi na kupata alama za juu kabisa.

Moja kati ya shule niliyofika huko mkoani Lindi nilimkuta kijana Aliyefanya mtihani wa hisabati ukiwa ni mgumu sana na akapata 42/50, Ukitafuta mazingira na maisha anayotokea ukihusisha na matokeo yake unaweza kuumia na kuguswa sana, utaumia zaidi ukifikiria Atapimwa na mtihani sawa na wanaofanya watoto wa majiji kama Dar es salaam,Arusha,Mbeya,Dodoma,Mwanza,na Manispaa kama Moshi, Kahama,Iringa,Bukoba n.k.

Nalishauri baraza la Mitihani la Taifa(NECTA)&Wizara ya Elimu kufikiria kutofautisha mitihani kulingana na Mazingira au kutofautisha kiwango cha Alama ambazo anapaswa kufikia mwanafunzi ili kuchaguliwa shule maalumu kulingana na mazingira na changamoto za mahali husika.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.