KUCHAGULIWA KWA KEISHA SOMO NYETI KWA WASANII WANASIASA

 

Na. Dady Igogo.

Kumekua na wimbi la wasanii kuingia kwenye siasa. Baadhi yao wamekua wakidhani kuwa maumbile yao, uzuri wao, mwili wao au umaarufu wao unaweza kuwafanya wakafanikiwa kwenye malengo yao ya kisiasa. Wapo pengine waliofanikiwa kwa hayo lakini yamekua ni mafanikio ya muda mfupi.

Msanii Keisha aliwahi kugombea ubunge wa viti maalum kundi la walemavu mkoa wa Dodoma na kushinda tarehe 26/07/2015. Lakini hakufanikiwa kwenye kundi la Taifa.

Ni dhahiri kuwa ukiangalia post zake, picha zake na namna alivyo na heshima utagundua kuwa kuchaguliwa huko siyo tu kwamba ni kundi la walemavu bali ana nidhamu, heshima, kutahamini utu wake kama mwanamke.

Wakati anagombea mwaka 2015 aliwahi kusema kuwa _mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali najipenda na ninajiamini lakini yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo tunastahili kuipata kutoka nchini kwetu_

Hiyo ndiyo imani aliyonayo Khadija Shabaan Taya maarufu kwa jina la Keisha. Alishawahi kufanya collabo na Msanii Diamond Platinum kwenye wimbo ulioitwa “nimechoka”.

Hongera sana Khadija Shabaan Taya!

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.