KANGI LUGOLA ATOA SIKU 10 KWA KAIMU MKURUGENZI NIDA KUFIKA OFISINI KWAKE DODOMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola ametoa siku 10 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Ndg. Andrew W. Massawe, kufika ofisini kwake Dodoma kutolea ufafanuzi baadhi ya mambo yanayohusu NIDA.

Lugola amemtaka Massawe kufika ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani jijini Dodoma akiwa na Wahusika wa kampuni ya Ideis Dilham.

Mhe. Lugola amesema lengo la kumuita Massawe afike ofisini kwake ni kwaajili ya kutolea ufafanuzi wa kwanini mitambo ya kuchapisha vitambulisho haijafika nchini mpaka sasa.

Aidha Mhe. Lugola amesema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili aweze kubaini nini tatizo kabla ya kuchukua hatua zaidi dhidi ya Kaimu Mkurugenzi huyo.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.