KANGI LUGOLA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KITUO CHA POLISI – MBAGALA

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. kangi Lugola siku ya leo Julai 14, 2018 amerfanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo cha polisi cha Mbagala Kizuiani kilichopo jijini Dar es Salaam.

Akiwa kituoni hapo waziri Lugola alipata fursa ya kuzungumza na mahabusu pamoja na kupitia mafaili ya baadhi ya mahabusu hao.

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akikagua baadhi ya mafaili

Katika ziara hiyo waziri Lugola amebaini mapungufu kadhaa katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kucheleweshwa kwa mahabusu hao kufikishwa mahakamani.

Tangu akabidhiwe majukumu ya kuiongoza wizara ya mambo ya ndani nchini, Lugola ameonekana kufanya ziara katika idara mbalimbali zinazohusu wizara hiyo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.