Kangi Lugola alivyomzuia Kamishina wa Magereza kuingia kwenye mkutano wake

Kamishina wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa amezuiwa kuingia kwenye mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola baada ya kuchelewa kwa dakika mbili kuingia kwenye ukumbi ambako mkutano huo ulifanyika.

Waziri huyo ambaye aliingia kwenye ukumbi majira ya saa 4:51 asubuhi ambapo mara baada ya kuingia aliagiza kwamba ikifika saa 5:00 mtu ambaye atakuwa hajaingia ukumbuni hataruhusiwa kuhudhulia kikao chake isipokuwa waandishi wa habari.

Ilipofika saa 5:00 aliagiza mlango ufungwe na usifunguliwe kwa mtumishi yoyote wa wizara wala Kamanda yoyote kuingia labda awe mwanahabari. Ambapo baada ya Dakika mbili aliingia Kamishna Jenerali, Dk Juma akiambatana na maafisa watatu aliwazuia kuingia licha ya kuomba msamaha kwa mara tano. Ilikuwa kama ifuatavyo;

Kangi: Nani anafungua mlango wakati nimesema mlango unafungwa, hakuna kuingia tena kwenye kikao changu?

Dk Juma: Samahani mheshimiwa

Kangi: Hakuna sahamani hapa

Dk Juma: Samahani mheshimiwa

Kangi: Hapana.

Dk Juma: Sahamani mheshimiwa.

Kangi: Hapana rudi nje nyinyi ni askari mmekuwa ‘trained’.

Dk Juma: Mheshimiwa nimewahi nimefika tangu saa tatu.

Kangi: Nikisema ni saa tano ni saa tano kwahiyo mwende nje wote ambao mmekuja wakati nimeshaingia kwenye kikao mwende nje, nyinyi ni maofisa tena wakubwa wa Jeshi la Magereza lazima tuwe na jeshi lenye nidhamu kwahiyo nenda nje nakuheshimu sana

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.