KABEJI INAVYOTIBU VIDONDA VYA TUMBO

Kabeji ni nini?

Kabeji ni aina ya mboga ya majani inayostawi kwa wingi Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, mara nyingi watu hutumia kabeji kama mboga na wengine hulikatakata na kulitengeneza saladi (kachumbali).

Ikumbukwe kuwa mbali na kabeji kutumika kama mboga lakini pia ni dawa nzuri ya Vidonda vya tumbo.

Pamoja na Kabeji kuwa moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo lakini pia Kabeji ina ‘lactic acid’ambayo husaidia kutengeneza amino asidi inayohamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo na hatimaye kutibu vidonda vya tumbo.

Kabeji pia ina kiasi kingi cha vitamini C ambayo imethibitika kuwa na faida kubwa kwa watu wenye vidonda vya tumbo vilivyosababishwa na maambukizi ya bakteria aitwaye ‘H. pylori. Pia majaribio yamethibitisha kuwa juisi ya karoti freshi inayo vitamini U mhimu kwa ajili ya kudhibiti vidonda vya tumbo.

VIDONDA VYA TUMBO

Ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo umeibuka kwa kasi hapa nchini na hivyo huku idadi kubwa ya waathirika wa tatizo hilo hawajui sababu hasa ya vidonga vya tumbo huku baadhi yao wakiamini kuwa, ni tatizo linalosababishwa na kukaa bila kula kwa muda mrefu.

Ukweli ni kwamba sababu kubwa ya vidonda vya tumbo ni dalili ya mwili kupungukiwa maji nani matokeo ya kuzidi kwa asidi (acid) mwilini kuliko alkaline.

TUANGALIA JINSI GANI KABEJI INAWEZA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO

MATARISHO:

Kabeji

*  Chukua Kabeji ulisafishe kwa maji ya uvuguvugu ili kuua vijidudu.

*  Kata kabeji nzima mara mbili na uchukuwe nusu yake, chukuwa karoti mbili na ukatekate vipande     vidogo vidogo na utumbukize vyote kabeji na karoti kwenye blenda na uvisage ili kupata juisi yake.

* Kunywa kikombe kimoja cha juisi hii kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi, mchana na jioni na kikombe kimoja kabla hujaingia kulala.

* Rudia zoezi hili kila siku kwa wiki kadhaa na hakikisha unatumia juisi freshi pekee na siyo ukanunue juisi ya kabeji au karoti ya dukani.

ONYO:

Kuwa mwangalifu unapoandaa juice ya kabeji kwa kuwa unakuwa na wadudu wengi wanaosababisha maambukizi ya minyoo na Typhode.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.