JESHI LAAMUA KULINDA VISIMA VYA MAFUTA KWA MANUFAA YA WALIBYA

Tripoli, LIBYA.

Afisa mmoja wa Libya aitwaye El Manzar al Kharrtosh, ametangaza kuwa wanajeshi wametumwa katika eneo linalojulikana kama Hilali ya Mafuta huko kaskazini mwa nchi, ambalo lina visima vikubwa zaidi vya mafuta na bandari kubwa za mafuta za nchi hiyo ili kudhamini usalama wa eneo hilo.

Afisa huyo anayehusika na masuala ya habari katika kikosi cha 73 cha wanajeshi watembeao kwa miguu chini ya kamanda mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Libya, amesema kuwa brigedi ya 165 ya wanajeshi watembeao kwa miguu imetumwa katika eneo la Hilali ya Mafuta kwa lengo la kuimarisha hali ya usalama

Bw al Kharrtosh, ameashiria hali ya mambo katika eneo hilo la Hilali ya Mafuta na kueleza kuwa kwa kuwepo vikosi vya wanajeshi na kutumwa askari wengine katika maeneo ya kandokando ya eneo hilo, hali ya mambo ni shwari huku doria zikiendelea katika maeneo kadhaa katika eneo hilo la Hilali ya Mafuta.

Kikosi hicho cha brigedi ya 165 ya wanajeshi waendao kwa miguu chenye makao yake makuu mashariki mwa Libya, kinatambulika kama moja ya vikosi vyenye nguvu kubwa katika upande wa makabiliano na ulinzi na vilivyojizatiti vyema kwa silaha na rasilimaliwatu.

Kabla ya kutekelezwa hatua hii, Shirika la Taifa la Mafuta la Libya lilikuwa limetangaza kwamba kufungwa kwa visima vya mafuta kutakuwa na athari mbaya kwa uchumi wa nchi hiyo, hususan huko kusini mwa Libya kwa sababu kufungwa kwa visima hivyo tajwa kwa siku kunasababisha hasara ya dola milioni 32 kwa uchumi wa Libya.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.