IGP SIMONI SIRRO AWAONYA WANAOTAKA KULIFUNDISHA KAZI JESHI LA POLISI.

 

 

Dar es Salaam

Kamanda Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro leo tarehe oktoba 20, 2018 amekutana na kuzungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuzungumzia juu ya tukio la kupatikana kwa Mfanyabishara Mohamed Dewji.

Akizungumza na vyombo vya habari IGP Simon Sirro amesema “Nyinyi ni mashahidi jana nimezungumzia hii press nikiwa na uhakika lakini kuna watu wachache ambao sijui nia yao ni nini?, tukijaribu kufanya wao wanatufundisha, kikundi hiki cha watu wachache ambao ndio wamejenga imani ya kutoliamini jeshi la polisi, wao ndio wanajifanya wanajua upelelezi na wanajua zaidi ya jeshi la polisi hata kufikia hatua ya kutufundisha sisi jeshi la polisi namna ya kufanya kazi tukiwashika wasitulalamikie”

Pia Kamanda Sirro ameeleza kuwa Mohammed Dewji amesema watekaji hao walikuwa na wasiwasi sana, baada ya kuona hawawezi kutoka, njia pekee ilikuwa ni kuliacha hili gari hapa majira ya saa saba usiku.Kwenye gari tumekuta silaha za kivita kama AK47, ‘Sub-machine gun’ na Bastola 3. AK47 ikiwa na risasi 19 na risasi 16 za Bastola” alisema IGP Simon Sirro

Akihitimisha Kamanda Sirro amelishukuru jeshi la polisi na “Niwashukuru polisi na vyombo vya usalama kwa kufanikisha hili, wakati mwingine haya matukio yatusaidie kutuunganisha, matukio haya yasitugawe, “Watu wetu wako kwenye hizo nchi, tunataka kuwaonyesha ukizoea Tanzania siyo mahali salama, kama walizoea kwenye nchi zao siyo hapa kwetu. Kuacha gari hii na silaha siyo mwisho wa upelelezi. Najua kuna Mtanzania mmoja, tuwapate tuzungumze nao lugha nzuri”

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.