FAHAMU KUHUSU UBAGUZI WA RANGI NCHINI MAREKANI.

Maandiko matakatifu ya dini zote yanasisitiza kwamba Mungu ni mmoja na yeye ndiye baba yetu sote tuliowanadamu na jinsi vile tulivyo ni kwa mapenzi yake Mola na sifa za uumbaji wake. Hili ni suala ambalo kila mmoja analifahamu na kulikiri katika imani yake. Hakuna asiyefahamu ya kwamba binadamu sisi tumeumbwa katika muundo wa aina moja lakini kimuonekano tuko tofauti. Sifaa kuu za sisi wanadamu kwanza kabisa uhai wetu unaambatana na upumuaji, zoezi hilo likiisha basi sifa ya kuwa binadamu hupotea na kuwa maiti. Lakini pia binadamu sisi sote tuna kichwa, shingo, mikono, tumbo, miguu ambavyo ni vya kuonekana kwa macho, achilia bahati mbaya kwa wale ambao walikosa viuongo ama kiungo kimojawapo lakini sifa kubwa inabaki kuwa sisi ni binadamu.

Utofauti upo tena ni mwingi. Kuna utofauti kimaumbile, kwanza kijinsia ambapo kuna mwanaume na mwanamke halafu tofauti zingine ni kama vile unene na wembamba, urefu na ufuoi, weupe na weusi na baadhi ya tofauti ndogondogo. Tofauti zote hizo zimekuwa za kawaida pamoja na kwamba huwa hazikosi vijichangamoto vya hapa na pale. Lakini kuna tatizo kubwa sana kwa upande wa tofauti za kirangi. Katika hili kuna makundi makuu mawili ya rangi japo kiuhalisia bado hainishawishi kama maneno hayo yanabebana na muonekano wa sisi watu. Kwa upande wa hili inasemekana kuna watu weupe (wazungu) na watu weusi (waafrika). Tofauti hii ya kirangi hakika imekuwa shida tangu na tangu ambapo Waafrika tumekuwa tukionekana ni daraja la mwisho katika kila nyanja achilia mbali tafiti mbalimbali ambazo zinathibitisha mwafrika kuwa mtu mwenye uwezo wa juu katika kila idara.

Nimependa kuzungumzia suala hili la ugomvi kutokana na rangi katika lile jina maarufu la ubaguzi wa rangi (racial discimination kwa kimombo). Afrika ilipata kutawaliwa miaka ya 1900 hasa baada ya vita ya kwanza ya dunia na watu wa magharibi, sababu kubwa ikiwa ni utajiri wa malighafi, hali ya hewa na uzuri wa Afrika. Vita ya kwanza ya dunia (1914-1918) iliiacha Ulaya katika hali mbaya kabisa ya kiuchumi, na kutokana na mazingira mabovu ya kwao kama si Afrika basi hali ingewawia vigumu na pengine hadi leo wangekuwa masikini wa kutupa. Lakini pia suala la biashara ya utumwa ya miaka ya 1600/1700 iliiharibu sana Afrika na watu wake kisaikolojia, Waafrika pia kutokana na ukarimu wao waliamini kwamba wazungu walikuja kwa ajili ya biashara halali lakini haikuwa hivyo. Tangu hapo ndipo dharau za wazungu juu ya Afrika na Waafrika wenyewe zilipokomaa na kujiamini wao ndo wao na hata Waafrika walipoanza kujitambua na kuonyesha ubora na uwezo wao ndipo Wazungu walizidisha chuki dhidi ya Waafrika. Wazungu hawajawahi kutaka kuiona Afrika ikifanya mapinduzi na kuitawala Dunia, na hapo ndipo ubaguzi wa rangi unapoanzia. Duniani kwa ujumla suala hili katika nchi za wanaojiita weupe limeshika hatamu achilia mbali kampeni za ukweli wa usoni na uwongo wa moyoni zikifanywa. Nchi nyingi sana barani Ulaya, Marekani na Asia manyanyaso dhidi ya weusi ni makubwa mno, kwa leo hebu tuangalie kidogo Marekani, na tujikite katika migahawa haswa kutokana na maandiko fulani ya bwana Aamna Mohdin.

Migahawa ya Marekani ambayo ina  muunganiko wa majimbo 25 yamekumbwa na matukio makubwa manne ndani ya siku 12 tu. Baadhi ya matukio hayo yalirekodiwa. Moja ya video inaonyesha kijana mmoja mweusi wa kimarekani akizongwa na kusukumwa sukumwa ikiwa ni pamoja na kukabwa shingoni huku kaning’inizwa ukutani na askari wakati akimdhibiti katika nyumba fulani ya huduma za chakula (waffle house) huko Warsaw, Carolina Kaskazini. Kijana huyo anaitwa Anthony Wall (22) anasema alichukuliwa akiwa  anelekea na mdogo wake pamoja na watu wengine wachache maeneo hayo. Anthony alieleza kwamba walipofika sehemu ya huduma walikuta meza zikiwa chafu wakaamua kuketi kwa meza moja, na mmoja wa wahudumu alipokuja akawahoji kwa nini wameketi hapo, alimjibiu “Hupaswi kutusemesha hivyo”, ndipo polisi akaitwa na alipofika akamkaba Wall shingoni akimsukumizia kwenye ukuta wa vioo kitu ambacho hakikuwa sahihi. “Sikufanya fujo yoyote kwa askari huyo na hakusema chochote kwangu bali alianza kunikaba tu na kunisukumiza kwenye dirisha”. Anthony kupitia video hiyo alisikika akimuamuru huyo askari amuachie lakini askari huyo alimuamuru arudishe mikono yake nyuma.

Pamoja na suala hili kuonekana lakini hakuna hatua yoyote ya msingi iliyokwishachukuliwa japo ofisi kuu ya polisi imeahidi kutafuta ushahidi zaidi pamoja na kutizama vyema video zaidi. Hiyo ni miongoni mwa hali ambazo watu weusi wengi wanakutana nazo hasa Marekani nchi inayofahamika dhahiri kuwa na watu weusi wengi na matajiri wenye nguvu kipesa.

Bernard King binti wa aliyhewahi kuwa mwanaharakati na mpiganaji wa haki za watu weusi miaka ya 1900 nchini marekani Martin Luther King Jr…alitweet kwamba watu wanatakiwa kuwa mbali na waffle house mpaka migahawa itakaporidhia kuajili wataalamu, kujadili ubaguzi na kutekeleza mabadiliko. 

Tukio hilo limekuja muda mfupi tangia tukio la mwanamke mweusi wa kimarekani alipokamatwa akiwa waffle house katka jimbo la Alabama baada ya kukataa kulipa  senti 50 kwa ajili ya kikontena cha plastiki  na kuomba namba ya kampuni. Chikesia Clemons alikandamizwa chini sakafuni na maaskari watatu nakuachwa hata pale upande mmoja wa nguo yake uliposhuka chini na kuacha maziwa yakiwa nje. Lakini kiongozi wao alisema polisi ambao walihusika hapo walifuata protoko, huku akieleza kwamba Clemons na rafiki zake walikuwa na vurugu ndani ya waffle house na kumsumbua muhudumu wa mgahawa wakiahidi ya kwamba wangerudi na bunduki. 

Katika kuthibitisha yote hayo yanafanywa kwa shinikizo la  ubaguzi wa rangi tujiulize, je ni kweli waafrika tu ndo wasumbufu na wenye vurugu?, je ni kweli watu weusi tu ndo sio waelewa?, ni kweli watu weusi tu ndo sio wastaarabu?, je watu weusi  hawapawi hata kubisha jambo lolote ili kupewa maelezo ya kina?, je ni kweli wahudumu wa restaurant hizo hawawezi kukabiliana wenyewe na watu weusi mpaka polisi?, Ina maana kazi yao hawana utaalamu nayo?

Lakini lazima tufahamu migahawa ya chakula ni moja ya sehemu za mikusanyiko ya watu wote wanaohitaji huduma ambayo imekuwa na msaada mkubwa kwa wamarekani wote, lakini suala ambalo linaendelea ndani ni hali ya Wamarekani wengi hasa kwa watu weusi kunyanyaswa,Waffle house imekuwa ni maeneo ya manyanyaso kwa muda mrefu sana kwa raia wake na hasa Wamarekani wa kusini  zaidi ya miaka 60, na malalamiko makubwa ni kwenye suala la ubaguzi wa rangi tofauti na matukio mengine. Kwa miaka 40 waffle house zimekuwa zikishitakiwa si chini ya mara kumi katika sekeseke hili.

Kwa mfano mwaka 1984, binti mmoja wa kizungu aliwahi kushitaki baada ya kufukuzwa kazi kisa kaolewa na mwanaume mweusi. 2001 kundi la muziki wa injili lilifungua jalada la kesi kuhusu waffle house kwa kuvunja haki za kiraia (civil rights). Mashitaka yao yalisema kwamba katika waffle moja Carolina Kaskazini waliwaamuru wasimame kwenye viti ili waweze kukaa wazungu baada ya kukosa siti. 2002 tena watu wawili waliishitaki waffle house baada ya kutembelea mgahawa mmoja  Columbus, Carolina Kaskazini hukohuko. Wapenzi hao walilalamikia suala la kutohudumiwa na wafanyakazi wa hapo. 2004 tena familia ya wamarekani weusi waliishita waffle house wakati huu Carolina Kusini baada ya mhudumu wa kike kudai kwamba mgahawa huo hauhudumii watu weusi. 2005 pia familia ya Waafrika wa Marekani walishitaki waffle house huko Georgia wakilalamikia pia kuzuiwa huduma kwa sababu ya rangi zao, familia hiyo asili yake ni Augusta huko Georgia huku pia kukiwa na masuala hayohayo mwaka 2006 ambapo kundi la mawarekani weusi walitoa malalamiko ya vitendo vya waffle house kunyanyasa waafrika katika kutoa huduma za chakula na nyinginezo. Kwa mfano ilielezwa kwamba Waafrika huwa hawahudumiwi na mara nyingine hata wakihudumiwa hutakiwa kulipa kwanza hali ambayo ni tofauti na wamarekani weupe.

Mwaka 2013 kuliwahi tokea shitaka la mfanyakazi mmoja wa waffle house kulalamikia kutengwa hata kazini huku akieleza kwamba wafanyakazi wawili wazungu walimbagua kwa ngozi na umri wake lakini hawakupewa onyo lolote. 2014 pia kukawa na mashitaka ya kutotendewa sawa na wafanyakazi wengine kwa mfanyakazi wa kiafrika mmoja alitoa malalamiko hayo. 2016 pia kukawa na kesi nyingine ambapo mwafrika mmoja  alilalamika ya kwamba mhudumu mmoja wa kizungu alikataa kuwahudumia na hata mwingine aliyewahudumia hivyohivyo. Lakini baadae lilikuja kundi kubwa la waendesha pikipiki akiwamo baba wa mhudumu aliyewahudumia wapenzi hao wakiafrika na wakaingia mgahawani na kuketi  pamoja karibia na wapenzi hao. Walipoondoka mgahawani  hapo wakaeleza kwamba waendesha pikipiki hao waliwafuata nje, ambapo baba yake na mhudumu wa kike aliyewahudumia alitoa kisu kuwatishia huku mhudumu huyo akiwaonyesha dharau.

Huo ni moja ya shahidi chache sana kuhusu hali ya Marekani nchi ambayo inajigamba kwa kuthamini na kuheshimu haki na utu wa raia wote. Ni dhahiri kumekuwa na ukakasi mkubwa sana katika kutoa hukumu ama maamuzi linapokuja suala la mtu mweusi kutaka haki Marekani. Tumeweza kuona hata kesi nyingi nchini Marekani zikiwahusu watu weusi kwa sana. Kwa mfano pamoja na ukweli wa mambo hebu fikiria kuhusu mzee Cosby mchekeshaji maarufu na wa kuheshimiwa Marekani, R Kelly mwanamuziki nguli Marekani, hebu tizama umaarufu wa hawa watu lakini kesi zao zimekuwa zikisimamiwa haswa hata kama mambo hayana ushahidi. Linapokuja suala la kesi za wazungu eidha wao kwa wao au dhidi ya Waafrika zimekuwa zikiisha haraka bila ya kuwa na mlolongo unaoweza kuwaathiri watu kiasaikolojia.

Suala la Kanye West kuongelea utumwa na uungaji wake mkono kwa Donald Trump unaweza kuona ni kwa kiasi kikubwa wamarekani wengi weusi wamekuja juu kwa sababu ni wazi Trump ni mmoja ya wabaguzi wakubwa kwani hajasita kuelezea mtizamo wake juu ya waafrika pamoja na kudai ya kwamba anasimamia ukweli lakini sio kweli. Hata kabla ya kuwa rais Trump aliwahi kueleza wazi kwamba Wamarekani weusi ndio changamoto kubwa Marekani kwani ni wapenda starehe lakini akasahau ni miongoni mwa makundi ya watu wanaoliingizia pesa nyingi sana taifa hilo kubwa ulimwenguni kwa malipo ya kodi kutokana na biashara kubwa ya sanaa wanayofanya.

Kuuawa kwa waafrika na maaskari weupe limekuwa jambo la kawaida na kumekuwa na ukakasi linapokuja suala la maamuzi ya hukumu. TIZAMA TAKWIMU CHINI: 

Mathalani 2016 askari anayefahamiaka kwa majina ya Michael T Slager alimpiga risasi na kumuua Walter L. Scott, 2015 Betty Jo Shelly alikutwa hana hatia  baada ya kumuua Terence Crutcher. Hayo ni baadhi ya matukio ambayo bado yamewaacha huru watuhumiwa.

Napenda kushukuru kwa wewe ambaye umechukua muda wako kusoma makala hili, naamini kuna fundisho kubwa sana ndani yake, kwanza itakupa kujua ukweli wa wale tunaoamini ni wenzetu na siku ukibahatika kwenda huko utachagua maeneo mazuri ya kwenda kwani ni dhahiri wazungu wengi hawapendi ukaribu ama hata kuonekana kulingana ama kuzidiwa na chochote na mwafrika. Naamini kuna mengi tafadhali niachie maoni yako, katika kesi hii ya hali ya ubaguzi nchini Marekani hasa  leo tukiwa tumeangazia zaidi migahawani.

 

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.