BONGE KUBWA LA BARAFU LASABABISHA TAHARUKI KUBWA KISIWANI GREENLAND

Taharuki kubwa imewakumba wakazi wa kijiji kimoja magharibi mwa Greenland mara baada ya bonge kubwa la barafu lililopo katika maji kuonekana katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa mamlaka za hali ya anga katika kisiwa hicho, bonge hilo lingeweza kusababisha mafuriko makubwa iwapo lingevunjika na mawimbi yake kuelekea katika nyumba za kijiji hicho.

Inasemekana kuwa barua hiyo ilikuwa na urefu zaidi ya urefu wa nyumba zinazopatikana kijijini hapo, na inasemekana pia barafu hiyo ilionekana kuganda hewani kwa kipindi cha siku moja.

Maafisa wa eneo hilo wanasema hawajawahi kuona bonge kubwa la barafu kiasi hicho.

Habari zaidi zinasema kuwa wanakijiji wapatao 169 wanaoishi karibu na bonge hilo la barafu, wamechukuliwa na mamlaka za mji huo kwaajili ya usalama zaidi.

”Kuna nyufa na mashimo yanayotufanya kuwa na hofu kwamba huenda bonge hilo likavunjika ,”, mwanachama wa baraza la kijiji hicho Susanne Eliassen aliambia gazeti la eneo hilo la Sermitsiaq.

Baadhi ya wataalamu wameonya kuhusu kutokea kwa mabonge mengi ya barafu kutokana na mabadiliko ya hali ya anga, hatua inayozidisha hatari ya kutokea kwa vimbunga vya Tsunami.

Mnamo mwezi Juni wanasayansi wa chuo kikuu cha New York walitoa kanda ya video ya bonge kubwa la barafu lililokuwa likivunjika mashariki mwa Greenland.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.