DONALD TRUMP:INAONEKANA JAMAL KHASHOOGI AMEUAWA

 

New York, MAREKANI.

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema inavyooneka, Mwanahabari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoogi, aliyetoweka akiwa ndani ya ubalozi wa nchi yake, nchini Uturuki, ameuawa.

Rais Trump amesema inasikitisha sana lakini anasubiri ripoti kamili kabla ya kutangaza hatua ambazo amesema zitakuwa kali kwa uongozi wa Saudi Arabia.

“Nafikiri ameuawa, inasikitisha sana, lakini tunasubiri matokeo ya uchunguzi, kufahamu kilichotokea,” amesema Trump.

Khashoogi alionekana akiingia kwenye ubalozi wa nchi yake jijini Instanbul Uturuki, lakini hakuonekana tena.

Saudi Arabia imekanusha kuhusika na madai ya kuuawa kwa mwanahabari huyo, ambaye amekuwa akiandika makala za kuukosoa uongozi wa Riyadh.

Marekani inasema itaichukulia hatua kali Saudi Arabia iwapo itabainika kuwa ilihusika.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.