CHIRWA ANZAA KAZI AZAM FC ATUPIA DAKIKA YA 89

Na Shabani Rapwi, Dar es salaam.

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Azam FC, Obrey Chirwa alisajiliwa hivi karibuni kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nagoon FC ya Misri.

Usiku wa leo Ijumaa ameanza rasmi kibarua chake ndani ya klabu hiyo,kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya Miaka 23 .

Mchezo huo wakirafiki Azam FC wameibuka na ushindi wa magoli 2-0, goli la kwanza likifungwa na nyota Enock Atta dakika ya 12′ kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji Ramadhani Singano kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Azam Fc anaongoza goli 1-0.

Na kipindi cha pili kilianza kwa kasi na mno dakika ya 55′ kulifanyika mabadiliko akatoka Bruce Kangwa na kuingia Mshambuliaji Obrey Chirwa, akitumia dakika 32 tu kufunga goli dakika ya 89′ na kukamilisha ushindi wa magoli 2-0.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.