SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA HUDUMA ZA AFYA

DODOMA. Mpango wa Taifa wa Damu salama umetakiwa kuhakikisha Hospitali Binafsi zote zinaanza kuchangia gharama za huduma za afya ili kupata mgao wa damu. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua mashine za kupima sampuli za damu na utendaji kazi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama. Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa ni lazima Mpango huo uhakikishe unajiendesha wenyewe na kuhakikisha unapunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali katika kutimiza majukumu…

Soma Zaidi >>

WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO YATOA TAMKO MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

Na Amiri kilagalila Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imewashukuru waganga wa tiba asili na tiba mbadala kwa ushirikiano katika afya za binaadamu na maendeleo ya jamii kwa ujumla huku serikali ikiendelea kutambua umuhimu wa fani hiyo muhimu na kuwataka waganga wa tiba asili kuendelea kutoa ushirikianao katika zoezi la uhakiki ili waweze kufanya kazi kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na wizara ya afya. Akizungumza na waganga wa tiba asili na tiba mbadala katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe kwa niaba ya katibu mkuu wa…

Soma Zaidi >>

KIKUNDI CHA VYAMA VYA SIASA CHAJITOSA KUSAIDIA DAMU HOSPITAL YA NYERERE

Na,Naomi Milton Serengeti Kikundi cha ujamaa na ujirani mwema Serengeti (KICHAUMWESE) kinachoundwa na vyama vitano vya siasa kimejitokeza na kuchangia unit 18 za damu kusaidia wahitaji mbalimbali katika Hospitali Teule ya Nyerere ddh Hospital hiyo bado ina changamoto kubwa ya uhitaji wa damu hasa kwa makundi maalum kama vile mama wajawazito na watoto lakini pia kwa watu majeruhi ambao hupata ajali Katika mkutano wao mkuu uliofanyika wilayani Serengeti wanakikundi walikabidhi hati ya usajili kwa katibu Tawala wilaya Cosmas Qamara aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na kuahidi kuendeleza…

Soma Zaidi >>

UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KAGERA, WENYE MATATIZO MBALIMBALI WAOMBWA KUJITOKEZA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UJIO WA MADAKTARI BINGWA NA KLINIKI TEMBEZI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA KUANZIA TAREHE O5 HADI 11 NOVEMBA, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti anapenda kuwataarifu Wananchi wa Mkoa wa Kagera na nje ya Mkoa kuwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wameandaa Kliniki tembezi ya Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali itakayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Government) kuanzia tarehe 05 – 11 Novemba, 2018. Ikiwa…

Soma Zaidi >>

MAKONDA ASAINI MIKATABA YA LISHE NA WAKUU WA WILAYA ZA DAR

Na Heri Shaaban Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wakuu wa Wilaya zote kuakikisha Manispaa zao zinafanya vizuri katika kuzingatia suala la lishe, na wanapoingia katika vikao vyao vya baraza la Madiwani suala hilo iwe sehemu ya ajenda kila siku. Akizungumza mkoani humo, jana na wakuu hao mara baada ya kutiliana saini hiyo, ambapo amesema katika wilaya zote tano, Temeke Iĺala na Kinondoni ndio zina idadi kubwa ya watoto hivyo, ni vyema wakaenda kutoa elimu ya lishe pamoja na kujikinga na Utapia mlo ili waweze kukabiliana na…

Soma Zaidi >>

KABEJI INAVYOTIBU VIDONDA VYA TUMBO

Kabeji ni nini? Kabeji ni aina ya mboga ya majani inayostawi kwa wingi Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga, mara nyingi watu hutumia kabeji kama mboga na wengine hulikatakata na kulitengeneza saladi (kachumbali). Ikumbukwe kuwa mbali na kabeji kutumika kama mboga lakini pia ni dawa nzuri ya Vidonda vya tumbo. Pamoja na Kabeji kuwa moja ya dawa bora za asili zinazoweza kutibu vodonda vya tumbo lakini pia Kabeji ina ‘lactic acid’ambayo husaidia kutengeneza amino asidi inayohamasisha utiririkaji wa damu kwenda kwenye kuta za tumbo jambo linalosaidia kuuongezea nguvu ukuta wa tumbo…

Soma Zaidi >>

KITUNGUU SWAUMU HUTIBU MAGONJWA 30

Kitunguu swaumu ni nini? Ni moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na muhimu sana kwa afya ya binadamu. Mbali ya kutumika kama kiungo katika chakula ili kuleta ladha nzuri kwa mlaji, Kitunguu swaumu kinatibu magonjwa mengi karibu 30. Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Watu wa mabara mbali mbali duniani, walianza kutumia Kitunguu swaumu kama viungo katika mboga na tiba takribani  miaka 6000 iliyopita. Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi…

Soma Zaidi >>