MWANAMKE AKIKUJIBU HIVI,KIMBIA HARAKA

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu. KWA MFANO: 1. Ukimtumia sms ”Mambo mpenzi wangu?” akikujibu ”mambo mabaya”, usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ”sina hela dear” 2. Ukimtumia sms ”Maisha yanasemaje kipenzi changu” akikujibu ”maisha magumu hubby wangu we acha tu” usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ”nimefulia mwenzio kama nini sijui” 3. Ukimtumia sms ”Mbona…

Soma Zaidi >>

MASWALI NA MAJIBU YA NAIBU WAZIRI MHE. ANGELINE MABULA KWENYE KUNDI LA TANZANIA YETU LA WHATSAPP

  Na Dinna Maningo. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakijiuliza maswali mengi juu ya maswala mbalimbali yanayofanywa na Serikali pamoja na changamoto kadhaa ndani ya jamii lakini maswali yao hukosa majibu kwakuwa hushindwa namna wanavyoweza kufikisha ujumbe kwa mamlaka husika. Pia wengine utamani maswali hayo yangejibiwa na Viongozi wa Serikali wakiwemo Mawaziri wa Wizara mbalimbali lakini kutokana na mazingira ya kuwawezesha kuonana ana kwa ana na viongozi hao wanashindwa kufikisha kero zao ili zitatuliwe. Kwa kutambua umuhimu wa uhuru wa mawazo kundi laTanzania Yetu kupitia mtandao wa Kijamii wa Whassap lililoanzishwa…

Soma Zaidi >>

SHANTELL-02

Na Pastory Raymond Ilipoishia….. Angesahauje mshtuko alioupata baada ya kujigundua mjamzito baada ya Mghana huyo kumkimbia? Angesahauje jinsi alivyojaribu kuitoa mimba ya Shantell na asiweze? Na Leo anamuona akiwa amemeea kama shina la mgomba. Tunda la mwanaume pekee aliyewahi kumpenda na kuwa naye mpaka sasa akiwa na umri wa miaka Arobaini na kenda. Inaendelea…. Mwanamke huyu wa makamo aliyekuwa mbele yake aliivua miwani yake na hivyo kuyafanya macho yake yaweze kuonekana na kumpa mawazo ya kuwa siku zilizopita mama huyu alikuwa kisu kikali kilichokata mioyo ya wanaume wengi. Shantell alikuwa…

Soma Zaidi >>

KWAHERI MFALME DROGBA.

MAKALA. Nikiwa mdogo sana mwaka 2004 ,nakumbuka nilikuwa shule ya msingi Mwalim Nyerere ,wilayani Kinondoni mkoani Dar es salaam. Nilikuwa napenda sana mchezo wa soka hila sikujua klabu gani ni sahihi kwangu kushangilia lakini nakumbuka nyumba yetu ilikuwa na watu wengi na wengi walikuwa mashabiki wa klabu ya Liverpool na Manchester united ni mimi tu ndio nilikuwa nimesalia kuchangua timu ya kushabikia nilikuwa napenda kuchagua timu inayocheza vizuri. Nakumbuka siku moja mzee wangu (Baba) aliniletea jezi mgongoni imeandikwa Pires na nikienda uwanjani kucheza mpira wa makaratasi wezangu walikuwa wananiita Pires…

Soma Zaidi >>

SIMULIZI: SHANTELL-01

Na Pastory Raymond Ilikuwa ni Jumatatu kama Jumatatu zingine. Pilika pilika zilikuwa nyingi Kama ilivyo katika miji mingi Duniani. Mwanzo wa wiki tena! Wanafunzi wanaonekana nadhifu, Kila mtu mjini anaonekana mwenye shauku ya kutekeleza adhma aliyojiwekea katika wiki mpya. Wakati wengine wakiwa wana adhma zao wengine walikuwa wana uchovu kwa kusakata rumba wikiendi na kunywa vileo mbalimbali. Huku wengine wakiilani kwanini Jumatatu ilifika mapema. Wengine wakifurahi hasa wafanya biashara ndogondogo ambao washitiri wao wengine ni wale waliopo maofisini kwani wikiendi huwa wapo majumbani mwao na hivyo kutokuambulia mia mbili mia…

Soma Zaidi >>

WARAKA WA KWANZA KWA VIONGOZI SERIKALINI NA WAZAZI WOTE NCHINI JUU YA KUKABILIANA NA JANGA LA USHOGA KUPITIA JICHO LA SAIKOLOJIA.

  MAKALA: Imeandaliwa na mwanasaikolojia, Hamis Abeid +255769808725 Muhitimu Chuo Kikuu Cha Dar es salaam 2017. Habari za wakati huu ndugu zangu viongozi, wazazi na waTanzania wote kwa ujumla, ama hakika Mungu ni mwema na anazidi kulibariki Taifa letu hili tukufu lililobarikiwa neema ndogo ndogo na kubwa kubwa ila pia changamoto za hapa na pale, nawasalimu sana kwa kauli ya amani na upendo. Kwenye huu waraka wangu mfupi nitazungumza namna gani kama Taifa kwa ujumla tunaweza maliza kabisa hili tatizo la mapenzi ya jinsia moja. Kwanza kabisa naomba tutambue ushoga…

Soma Zaidi >>

NYUMA YA GARI KULIKONI RUSHWA BADO KIZINGITI CHA USALAMA BARABARANI?.

  MAKALA: Na, Jasmine Shamwepu. Ilikuwa siku tulivu ya Alhamisi majira ya saa nne asubuhi nilipoanza safari yangu kutoka Dodoma kuelekea Bagamoyo kupitia Jiji la Dar es salaam. Niliitwa kuhudhuria mafunzo ya usalama barabarani, yaliyokuwa yakiendeshwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ubia na Shirika la Afya Duniani (WHO). Nikiwa najiandaa kwa safari niliweka mizigo yangu kwenye buti na kuelekea kwenye kiti namba 6 kilichokuwa upande wa kushoto wa dereva kando ya dirisha. Nilipendelea kukaa karibu na dirisha kama abiria wengine wanavyokimbilia dirishani. Baada…

Soma Zaidi >>

GAMBOSI KIJIJI KILICHOSIFIKA KWA UCHAWI CHAFANYA MAPINDUZI YA MAENDELEO

  Na Dinna Maningo,Bariadi. Ukifika Kijiji cha Gambosi Kata ya Gambosi maarufu (Gamboshi)kilichopo km 50 Magharibi mwa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu utakutana na madhari nzuri yenye kuvutia iliyo sheheni miti ya kijani ya asili. Pia kuna hewa safi na maeneo mengi yaliyowazi huku maeneo mengine zikionekana  Nyumba za wananchi,mazao ya Pamba Mpunga,Mahindi na Viazi,Njegere,Choroko na Mbaazi. Kijiji hiki kwa miaka mingi Watanzania walio wengi wamekuwa wakiwa na hofu wakiamini kukithiri kwa imani za ushirikina na uchawi jambo ambalo linaelezwa kuwa kwa sasa hakuna uchawi imebaki tu historia au hadhithi…

Soma Zaidi >>

MAKALA:UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO MJINI WAKULIMA WAPANDA MBOGA KWENYE MIFUKO

Na Dinna Maningo,Mwanza. Naianza safari hadi mtaa wa  Magaka Kata ya Kahama wilaya ya Ilemela km 16 kutoka Jijini Mwanza  Kaskazini Magharibi mwa nchini ya Tanzania ili kufahamu ni kwanini wakulima wameamua kupanda mboga ndani ya mifuko na kwenye vichuguu pamoja na kujua namna kilimo kinavyowasaidia katika kupunguza tatizo la uhaba wa mboga za majani. Wanafunzi wa shule ya msingi Kahama wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wakimwagilia maji kichuguu walichokiandaa ili kupanda mboga za majani. Nafika hadi shule ya msingi Kahama Kata ya Kahama  naona kundi la wanafunzi wakiwa wamevaa sare za…

Soma Zaidi >>

UNUNUZI WA ZAO LA KOROSHO BADO NI KITENDAWILI

Umefanyika Mnada mwingine wa korosho November 4,chini ya usimamizi wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI katika kijiji cha Mnero Ngongo wilayani Nachingwea mkoani Lindi. Kati ya Zaidi Ya Tani Elfu tisa zilizopigwa mnada,ni Tani 50 tu zimeuzwa na wakulima wa Ruangwa,Nachingwea na Liwale kwa bei ya Tsh.3001 kwa kila Kilo. Kampuni moja ya Korosho Africa pekee imejitokeza kununua, huku mwenyekiti CBT,Mama Anna Abdallah akigusia mpango wa wabanguaji kuruhusiwa minadani ili wanunue korosho kwa bei ya juu ya mnada husika. Bado wakulima wanaendelea kulalamikia kinachoendelea kwani ni wazi siku zinakwenda…

Soma Zaidi >>