OFISI YA WAZIRI MKUU WASAINI MIKATABA NA MAKAPUNI YA VIJANA YATAKAYOTOA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imesaini mikataba na makampuni ya vijana yatakayoanza kujenga na kutoa mafunzo ya kilimo kupitia kitalu nyumba (Green House). Hafla hiyo ya utiaji saini mikataba hiyo ilifanyika Novemba 27, 2018 katika ofisi hiyo iliyopo jijini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga alisema kuwa serikali imetoa fursa kwa vijana kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia mradi huo utakao wawezesha kiuchumi na kuwaletea maendeleo katika jamii. “Malengo mahususi…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA AIPONGEZA ANSAF KWA KUCHOCHEA MAENDELEO YA KILIMO NA VIWANDA

Dar es salaam. Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Eng Stella Manyanya, amesema, endapo kutakua na ustawi wa sekta ya viwanda na kilimo nchini Tanzania, kutaokoa dola za kimarekani millioni 420 kila mwaka ambazo hutumika kuagiza chakula nje ya nchi. Kauli hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wadau wa kilimo na viwanda ulioandaliwa na jukwaa huru la wadau wa kilimo lisilo la kiserikali (ANSAF ) ambao umefadhaliwa na SDC, Irish Aid na UKAID kupitia KPMG. Amesema, Tanzania imekuwa ikiagiza maziwa, ngano, kuku na…

Soma Zaidi >>

KAMPUNI YA RUAHA FARM NI MKOMBOZI WA WAFUGAJI NYUKI IRINGA

KAMPUNI  ya  uchakataji  wa  asili  ya Ruaha farm  mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha  Honey  imeanza  kuwaokoa  kiuchumi  wafugaji wa  nyuki  mkoani Iringa kwa kutoa  mizinga na  kuwaunganisha na  soko la asali . “kampuni  ya Ruaha Farm  imekuja  kivingine  baada ya  kufunga mashine  za  kisasa  za  kuchakata  asali  yenye  ubora pasipo  kutumia vifaa vya  kienyeji kama moshi  na vingine “  Mkurugenzi  mtendaji wa kampuni ya Ruaha  Honey  Fuad Abri  alisema  kuwa  kampuni yake  imeendelea  kuunga mkono jitihada za  serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya   Rais Dkt  John Magufuli ya Tanzania  ya  viwanda .  Alisema ubora wa  asali  ya kampuni ya Ruaha Honey  ni tofauti na  asali   nyingine  zinazouzwa  mitaani kwani  sifa  kubwa ya  asali  ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park.  Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi…

Soma Zaidi >>

DC HOMERA AAGIZA KUPITIWA UPYA DAFTARI LA WAKULIMA WA KOROSHO

Tunduru. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera ameagiza wataalamu wa kilimo, Maafisa ushirika, viongozi wa AMCOS Watendaji wa vijiji na Kata pamoja na maafisa Tarafa kupitia upya orodha ya wakulima wa korosho kwenye AMCOS na Katika vijiji mbalimbali. Agizo hilo alilitoa October 4 mwaka huu katika kikao cha kazi kilichoitishwa na Bodi ya korosho Tanzania CBT, Kilichofanyika mkoani Mtwara kufuatia kuwepo kwa dalili za majina hewa katika madaftari ya wakulima wa korosho. Aidha DC Homera amesema kuna baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji wamejiorodhesha majina yao kama wakulima…

Soma Zaidi >>

MADALALI WA KOROSHO KWA WAKULIMA WAPIGWA MARUFUKU MTWARA

Na Omary Hussein,Mtwara. Serikali wilayani Mtwara imewatahadharisha madalali wenye tabia za kuwalaghai wakulima na kununua Korosho kabla ya msimu kuanza kwa kuwataka kutafuta kazi nyingine za kufanya kwani katika msimu huu wa mwaka 2018-2019 kumewekwa utarabitu madhubuti kuhakikisha watakao ruhusiwa kuuza Korosho ni wakulima wenye mashamba yanayo tambulika katika wilaya hiyo. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mtimwilimbwi Halmashauri ya mji Nanyamba waliojitokeza katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi. Akiwa…

Soma Zaidi >>

WAFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA RUNGWE WAOMBA ASAS AWAJENGEE KIWANDA.

WAFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA RUNGWE WAOMBA ASAS AWAJENGEA KIWANDA. Na Rashid msita, Mbeya. Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya, wamemuomba mnunuzi wao wa maziwa namba moja wilayani humo ASAS, kuwajengea kiwanda cha maziwa ili kuongeza thamani ya bei ya maziwa yao. Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha MUWAMARU, Bw John Mwamfupe, amesema hayo leo Septemba 07, katika mkutano wa wafugaji uliofanyika wilayani hapo, ambapo ameomba uongozi wa ASAS kuwajengea kiwanda cha maziwa wafugaji hao kwa kuwa wamekuwa wakizalisha maziwa mengi kuliko wafugaji wa wilaya nyingine yeyote…

Soma Zaidi >>

WANANCHI KILUMBU WILAYA YA KILOLO WALIA NA AFISA MIFUGO NA KILIMO

WANANCHI  wa kijiji  cha Kilumbu  kata ya  Ibumu  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  wadai  ofisa  mifugo  amekuwa  si  msaada   kwa  wafugaji  wenye  uhitaji  wa  huduma  ya kupatiwa  tiba ya  mifugo yao  ila  amekuwa  mwepesi kukikimbilia  kwenda  kupima  nyama inapochinjwa  ili  kupewa  kitoweo. Wananchi hao   watoa  malalamiko  hayo  kwenye  mkutano  wa  asasi   isiyo ya  kiserikali ya Mazombe Mahenge Development Association” (MMADEA) wakati  wa mkutano  wa  hadhara  wa  lengo la ushiriki wa  wananchi katika  usimamizi  wa  uwajibikaji  katika wilaya ya  kilolo ,kwenye  kata za Idete,Ibumu ,Uhambingeto na  Nyanzwa . Walisema  kuwa  wanaomba  maofisa  ugani…

Soma Zaidi >>

WAKULIMA WA KARANGA MAHENGE WILAYANI KILOLO WALIA NA SOKO

Wakulima wa zao la Karanga na mtama katika kata ya Mahenge wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wameiomba serikali kusaidia kutafuta soko la mazao hayo. Wakulima hao walimweleza Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah wakati wa mkutano wa hadhara Jana kuwa wamekuwa wakirudishiwa karanga kutoka Dar es Salaam kwa madai soko hakuna. Shaban Omari alisema kuwa kutokana na kukosekana kwa soko la uhakika wakulima wa zao la Katanga na Mtama wameanza kuhofu kulima kilimo hicho hivyo kuomba serikali kuwatafutia wanunuzi wa uhakika . Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya…

Soma Zaidi >>