NAIBU SPIKA TULIA ACKSON AWAPA NENO VIONGOZI WA UVCCM.

  Dodoma. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Akson hii leo amezungumza na Viongozi mbalimbali wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi katika Semina Inayoendelea Jijini Dodoma. Akizungumza na Viongozi hao Mhe. Naibu Spika Tulia Akson amewaomba Viongozi hao kuendelea kufuatilia Utekelezaji wa Ilani ya CCM ili kuendelea kuisaidia Serikali ya awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ili kutekeleza ahadi zake. Pia Mhe. Naibu Spika ameupongeza Umoja wa Vijana…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE.KANYASU AWAOMBA WATUMISHI WAMPE USHIRIKIANO

    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu amewaomba watumishi wa Maliasili na Utalii wampe ushirikiane ili aweze kutekeleza majukumu kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John pombe Magufuli amemuamini na kumteua ili aweze kuitumikia Wizara hiyo. Ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwa mara ya kwanza na Watumishi hao mara baada ya kuwasili makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dodoma Amewaomba watumishi hao wampe ushirikiano na pale mafanikio yanapopatikana yanakuwa ni mafanikio ya wizara nzima na sio ya kiongozi pekee. ‘’Mimi ni mgeni…

Soma Zaidi >>

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA KUMUUA MZEE WA MIAKA 60.

  Na Allawi Kaboyo,Kagera. Watu watatu wakiwamo mgambo wawili, wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumpiga na kumuua mzee mmoja aitwaye Daud Rwenyagira (60) mkazi wa kijiji Nyakahita wilayani Karagwe, baada ya kumtuhumu kuwazuia kufanya kazi yao ya kumkamata mtu aliyekula fedha za manunuzi ya kahawa. Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Kagera,Revocatus Malimi amesema kuwa mgambo hao walitumwa na mtendaji wa kijiji Nyakahita, kwenda kumkamata Theophil Pima, baada ya kulalamikiwa na mama aitwaye Mali Byamanyirwohi aliyemtuhumu kula hela zake za kununulia kahawa (BUTURA) na…

Soma Zaidi >>

MBEZI FUN RUN YAPANIA KUDUMISHA AMANI NA UPENDO NCHINI

Mbio za ‘Mbezi fun run’ zimepania kudumisha amani na upendo hapa nchini kuelekea mwisho wa mwaka na kuboresha afya za watanzania. Hayo yamesemwa hii leo na Omary Kimbau msemaji wa Mbezi fun run group ambao ndiyo waandaaji wa mbio hizo kwa wakazi wa maeneo ya Mbezi na Dar es salaam kwa ujumla kushiriki mbio hizo kwa lengo la kudumisha amani iliyopo nchini pamoja na kuboresha afya zao. “Tumeona ni busara mwisho huu wa mwaka sisi wa Mbezi tuungane kwa pamoja katika mbio hizi na matembezi ikiwa kama ni sehemu yetu…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA ROSTAM AZIZ, MBATIA,CHEYO NA SHIBUDA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Novemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na wanasiasa Mhe. John Cheyo, Mhe. James Mbatia na Mhe. John Shibuda, na mfanyabiashara Bw. Rostam Aziz Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo hayo Bw. Rostam Aziz amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi bora ambapo amesema anatengeneza misingi imara ya uchumi unaokua kwa uhakika zaidi kwa kujenga miundombinu ikiwemo barabara, reli na bandari ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi na kuzalisha ajira. Bw. Rostam Aziz amesema…

Soma Zaidi >>

DKT. MPOKI AELEZA UCHOVU SABABU ZA AJALI BARABARANI NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa moja ya sababu za ajali barabarani, ni uchovu wa madereva. Dkt. Mpoki ameyasema leo Novemba 13,2018 wakati wa kufungua mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya Hospitali nchini. Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Dkt. Mpoki amelitaka jeshi la Polisi nchini kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa madereva kubadilishana kwani suala la uchovu linachangia kwa kiasi kikubwa ajali za…

Soma Zaidi >>

SIKU MOJA BAADA YA KUAPISHWA WAZIRI WA KILIMO NA TIMU YAKE WAMEWASILI MKOANI MTWARA KUFUATILIA MASUALA YA KOROSHO.

  Na,Bakari Chijumba,Mtwara. Ikiwa ni siku moja tu mara baada ya kuapishwa kuongoza wizara ya kilimo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam Jana Jumatatu Novemba 12, 2018, Waziri wa kilimo Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) Leo. Novemba 13, 2018 ameongoza viongozi wakuu wa Wizara yake kutembelea katika Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa ajili ya kuhakiki Korosho zilizopo katika maghala makuu. Katika msafara huo Mhe. Waziri Hasunga atatembelea Mkoani Mtwara ambapo ameambatana na Naibu Waziri wa kilimo Mhe. Innocent Lugha Bashungwa na Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe watakaotembelea…

Soma Zaidi >>

RC SONGWE ATOA SULUHU MGOGORO WA UCHIMBAJI MADINI

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wamesuluhisha mgogoro baina ya wakazi wawili wa kijiji cha Saza Wilaya ya Songwe kuhusu eneo la uchimbaji wa madini. Brig. Jen. Mwangela amesema Suzan Karan amebainika kisheria kuwa ni mmiliki halali wa eneo lililokuwa likigombewa kwa kuwa ana leseni halali huku Elimbotwa Naftari ambaye hana leseni na amekuwa akidai umiliki wa eneo hilo amebainika kuendesha shughuli za uchimbali kinyume na sheria. Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus E. Mwangela…

Soma Zaidi >>

MDAMI: BILA KITAMBULISHO CHA TAIFA HUWEZI KUPATA HUDUMA YEYOTE NCHINI.

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), imesema kuwa huduma nyingi kwa sasa zinategemea vitambulisho vya taifa na hayo yanafanyika ili kuongeza msukumo wa watu kufatilia vitambulisho hivyo. Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio msemaji wa NIDA, Rose Mdami amesema kuwa mamlaka hiyo inataka kila mtu mwenye umri wa miaka 18 awe na kitambulisho, kwani matumizi yataongezeka zaidi ya hapo. “Mpaka sasa tumeshaandikisha wananchi milioni 19, na lengo tufike zaidi ya hapo na adhma yetu kila Mtanzania awe na kitambulisho cha taifa ili iwe rahisi kutambuana,…

Soma Zaidi >>

DIWANI WA VITI MAALUM MANISPAA YA ILALA NEEMA NYANGALILO ATEMBELEA YATIMA.

Na Heri Shaaban. Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangalilo amesherekea miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Magufuli kwa kugawa vyakula katika kituo cha watoto Yatima Msimbazi wilayani Ilala. Katika hafla hiyo ya kutembelea watoto yatima wa Msimbazi Diwani Neema aliongozana Umoja wa Wanawake wa( UWT) kata ya Ilala. “Mimi kama Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala nimpongeza Rais wangu Magufuli katika uongozi wake pia nimetumia siku ya leo kushiriki katika kituo cha Msimbazi kuwaona watoto na kuwapa misaada”alisema Neema. Neema alisema msafara wake alikuwa…

Soma Zaidi >>