MAKAMANDA WA POLISI MIKOA MITATU WATENGULIWA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametengua uteuzi wa makamanda wa polisi wa mikoa mitatu; Salum Hamduni (Ilala), Emmanuel Lukula (Temeke) na Ramadhani Ng’azi (Arusha). Ametangaza uamuzi huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza. Amesema sababu za kutengua uteuzi wa kamanda wa Ilala na Temeke ni kushindwa kusimamia mianya ya rushwa na utoaji wa dhamana kwa watuhumiwa. Pia, amemuagiza katibu mkuu wa wizara yake kuunda kamati ambayo itapewa miezi mitatu kuchunguza vitendo…

Soma Zaidi >>

BREAKING NEWS: MFANYABIASHARA MWINGINE WA KIHINDI ATEKWA TABORA

    TABORA: Mfanyabiashara mwingine mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika kwa jina la Kishori ametekwa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 25, 2018 na kisha kuondoka nae sehemu isiyojulikana. Kwa mujibu wa mashuhuda ambao wameongea na mwandishi wa mtandao wa Dar Mpya mapema leo mjini hapa, wameeleza kuwa, tukio hilo limetokea eneo la katikati ya mji wa Tabora karibu na Golden Eagle hotel eneo ambalo ni jirani na ofisi na makazi yake. Shuhuda hao wameongeza kuwa, wakati tukio hilo limetokea lilikuwa ni la ghafla na walimchukua na kisha kukimbia na…

Soma Zaidi >>

WATU 16 WANAODAIWA KUWA NI WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA ILALA

  Naibu Kamishna uhamiaji, Afisa uhamiaji Ilala Pili Zuberi Mdanku kwa kushirikiana na OCD Ilala SP Jason Ibrahim wamefanikiwa kuwakamata watu 16 wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu katika kata ya Mchikichini Jimbo la ilala. Hatua hiyo, imekuja mara baada ya mmoja wa wananchi kutoa kero kwa mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuwa kuna nyumba ambayo inawahifadhi wahamiaji haramu. DCI Pili ameamua kufanya doria katika eneo hilo mara baada ya kupata taarifa hizo kwani, si mara ya kwanza kufanya doria katika eneo hilo na kuwakamata wahamiaji haramu. Amesema kuwa,…

Soma Zaidi >>

BASI LA NEW FORCE LATUMBUKIA MLIMA KITONGA.

    Watu kadhaa wamenusurika kifo katika ajali iliyotokea hii leo katika mteremko wa Mlima Kitonga mkoani Iringa baada ya basi la kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es salaaam kugongana na gari nyingine linalodaiwa kuwa ni la kampuni ya Golden deer lilikuwa likitokea Dar kwenda Tunduma na kisha kuanguka chini ya mlima huo wenye mteremko mkali. Kaimu kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa , Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa za awali zinasema kuna majeruhi tu.

Soma Zaidi >>

HUKO AMERIKA NCHI 03 ZAOMBA MSAADA KUKABILIANA NA WAKIMBIZI

Nchi tatu za Kusini mwa Amerika, Colombia, Peru na Ecuador zinaomba msaada zaidi wa kimataifa ili kukabiliana na ongezeka la wahamiaji kutoka Venezuela ambao wanazidi idara zao za huduma kwa umma, mwakilishi wa Peru amesema baada ya mkutano wa pamoja huko Lima kuhusu wahamiaji. Nchi hizi tatu zimepokea mamia ya maelfu ya Wavenezuela wanaokimbia mdororo wa kiuchumi na kisiasa nchini mwao, ambako raia wamekua wakijiwezesha wenyewe kwa kupata chakula na kuondokana na matatizo ya maisha ya kila siku. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Wavenezuela zaidi ya Milioni 1.6, wameitoroka…

Soma Zaidi >>

MWENYEKITI NA MAKAMU WAKE KAMATI YA BUNGE YA BAJETI WAJIUZULU

DODOMA. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Abdulrahman Ghasia na pamoja Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Vrajlal Soni wamejiuzulu nafasi hizo. Katibu wa Bunge ndugu Stephen Kagaigai, akizungumza na mtandao wa Dampya.com hivi leo Agosti 28, 2018 amethibitisha taarifa hizo za kujiuzulu kwa viongozi hao katika kamati hiyo. “Mpaka sasa hatujajua sababu za wao kujiuzulu lakini ni kweli wamejiuzulu nafasi zao.” amesema Kigaigai Mh. Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini (CCM) pamoja na Soni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini naye CCM, wametangaza…

Soma Zaidi >>

“MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. JOKATE MWEGELO KUJA NA MBINU MPYA ZA KUINUA ELIMU KISARAWE. “

Na.. Mwalimu Richard Augustine Baruapepe: augustinerichard629@gmail.com +255754728801. Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi JOKATE MWEGELO leo tarehe 23/08/2018 amefanya kikao wilaya Kisarawe katika ukumbi wa mikutano uliopo wilayani hapo chenye lengo la kuinua Elimu katika wilaya ya Kisarawe. Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alianza kwa kuwatambulisha wadau mbalimbali walioamua kuunga mkono jitihada zake na jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wake Dr JOHN POMBE MAGUFULI ,alipongeza na kuwashukuru kwa kazi kubwa ambayo wameifanya ya kuamua kuleta baadhi ya vifaa mbalimbali ikiwemo Mashine ya…

Soma Zaidi >>