BREAKING NEWS :BASI LAIGONGA TRENI NA KUUWA WATU 7 NA MAJERUHI 27 MKOANI KIGOMA

Na Joel Silver

Watu 7 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo ambalo linafanya safari zake kutoka Mkoani Kigoma kwenda Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi.

Dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa watu waliofariki, huku idadi ya vifo ikitajwa kuweza kuongezeka, kutokana na majeruhi wengi kuwa kwenye hali mbaya.

Kamanda Otieno amesema kwa sasa jeshi la polisi lipo eneo la tukio likiendelea kuokoa miili na majeruhi wengine, na taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.

Endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ya darmpya.com ,@darmpya @dar_mpya na pia Youtube chaneli yetu ya darmpya  tutaendelea kutoa taarifa kwa kadri zinavyotufikia kutoka katika vyanzo vyetu rasmi

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.