BOBI WINE AIBUKA TENA, ALISHTUMU JESHI LA POLISI UGANDA KUTUMIWA KISIASA

 

 

Kampala, UGANDA.

Mbunge wa upinzani ambaye pia ni Mwanamuziki nchini Uganda Bobi Wine, amewashtumu Polisi kwa kuzuia tamasha aliloandaa mwishoni mwa juma hili jijini Kampala.

Polisi wanasema wameamua kusitisha tamasha hilo ambalo lilitarajiwa kufanyika katika uwanja wa michezo wa Naambole kwa sababu, hajafanya maandalizi ya kutosha na wasimamizi wa uwanja huo.

Hata hivyo, mbunge huyo ambaye amejipatia umarufu siku za hivi karibuni, na kuoneakana kupendwa na vijana wengi nchini humo, amesema serikali inahofia ushawishi wake hasa kwa vijana.

Bobi Wine, ambaye jina lake kamili ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka ya uhaini kutokana na kupigwa mawe msafara wa Rais Yoweri Meseveni wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo.

Bobi Wine alitarajia kutumia tamasha hilo kuzindua album yake mpya inyofahamika kama Kyarenga.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.