BABA MZAZI AMBAKA MWANAE WA MIAKA 7

Nairobi. Msichana mwenye umri wa miaka saba amelazwa katika hospitali ya kata ya Marimanti nchini Kenya kudaiwa kubakwa na baba yake mzazi

Akizungumza kutoka hospitali ambako alikuwa amempaleka msichana, mama wa binti huyo anasikitishwa na kitendo cha baba huyo kumnajisi mwanae taarifa iliyothibitishwa na afisa wa kliniki   ya Bernard Mwenda kuwa amebakwa.

Alisema mumewe alikuja nyumbani jioni na kuanza kugombana juu ya mtoto wao wa mwezi mmoja akisema kuwa hakuwa wake, aliimwaga chakula ambacho mke wake alikuwa amemtayarishia na kuanza kumpiga makofi na mateke.

“Sikuweza kuvumilia hili na nililazimika kukimbilia kwenye vichaka vya karibu. Wakati huo ambao sikuwepo alianza kuwapiga watoto wengine na kumtia unajisi msichana kabla ya kukimbilia, “ alisema Mama

Ilikuwa baada ya hayo mama wa msichana alikuja na kumpeleka hospitali. Afisa wa kliniki Bernard Mwenda ambaye alimhudumia msichana alisema uchunguzi ilithibitisha msichana alibakwa.

“Msichana alikuwa na mipasuko katika sehemu zake za siri lakini tunahitaji uchunguzi zaidi ili kujua kiwango cha majeruhi yake. Tunaweza kulazimishwa kumpeleka hospitali ya rufaa ya Chuka kwa matibabu zaidi,” alisema.

Mama wa msichana pia ana hofu kuwa mumewe anaweza kurudi wakati akiwa hospitalini na kuendelea kuwatendea ukatili watoto wake wengine.

“Ningependelea watoto kupelekwa mahali salama na polisi au hata Wasamaria wema kwa sababu anaweza kurudi na kuwatenda vibaya wengine wawili,” alisema.

Mkurugenzi wa polisi wa Tharaka wa Kusini Walter Abondo alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa harakati za kumsaka mtuhumiwa tayari zimekwisha anza.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.