DIWANI KATA YA MWANGATA AKUTANA NA WATUMISHI WA UMMA

NA FRANCIS GODWIN ,IRINGA Diwani wa kata ya Mwangata jimbo la Iringa mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Edward Nguvu Chengula amekutana na watumishi wa umma kata ya Mwangata kupata mipango kazi yao. Diwani Chengula amekutana Leo na watumishi hao katika ofisi ya kata ya Mwangata ikiwa ni mwendelezo wa vikao vyake vya ndani na watumishi wa umma kwa ngazi mbali mbali. Akizungumzia kikao hicho amesema kuwa toka achaguliwe kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni amekuwa akikutana na watumishi hao ili kupokea changamoto zao na mikakati ya kiutendaji kazi ili…

Soma Zaidi >>

DIWANI WA KATA YA MWANGATA KUJENGA CHUO KIKUU BINAFSI

  Na Francis Godwin, DIWANI wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Mwangata katika Manispaa ya Iringa Nguvu Chengula anakusudia kujenga chuo kikuu binafsi katika eneo la Kitasengwa ili kuongeza idadi ya vyuo zaidi katika mkoa wa Iringa. Chengula ambae ni Diwani aliyechaguliwa hivi karibuni kwenye uchaguzi mdogo wa marudio, Aliyasema hayo jana wakati wa mahafali ya darasa la saba katika shule ya Sun Academy, kuwa ujenzi wa chuo hicho utapanua wigo zaidi ya elimu ndani ya Mkoa wa Iringa . Amesema serikali iliyopo madarakani imejipambanua kuwa ni serikali ya…

Soma Zaidi >>

RC HAPI AAGIZA KAIMU MENEJA TANESCO IRINGA AWEKWE MAHABUSU

Na Francis Godwin Darmpya Iringa Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ameliagiza jeshi la Polisi kumkamata na kumweka mahabusu masaa mawili kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Iringa kwa kutoshiriki ziara yake. Hapi ametoa agizo hilo leo katika kijiji cha Kingonzile baada ya Diwani wa kata ya Nduli Bashiri Mtove kuwakilisha kilio cha wananchi wa kigonzile juu ya kuomba kusogezewa umeme . Kabla ya kujibu ombi la wananchi ambao walimsimamisha kutoa kilio hicho kupitia diwani wao ,mkuu wa mkoa alilazimika kumwita Meneja wa Tanesco ila hakuwepo na ndipo alipompigia…

Soma Zaidi >>

Amref TANZANIA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA AFYA NCHINI

  Na Francis Godwin,Darmpya Dodoma Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na masuala ya Afya (Amref ) Tanzania limetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za afya kwa mikoa mbali mbali nchini . Katika mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo katika ukumbi wa Dodoma Hotel jijini Dodoma ,mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Amref Tanzania  Josiah Otege, amesema kuwa shilika la Amref Tanzania  lipo nchini toka mwaka 1957. Amesema kuwa Amref  inajumla ya miradi 23 inayofanya kazi nchini na tayari imesambaa katika mikoa 15 nchini,ambayo imekua ikiwaletea maendeleo kutoka na…

Soma Zaidi >>

RC HAPI AIBUA UOZO MACHINJIO YA KISASA IRINGA MJINI AAGIZA CAG KUCHUNGUZA

Na Francis Godwin,Darmpya Iringa MKUU  wa  mkoa  wa Iringa Ali  Hapi ameagiza mradi wa machinjio ya  kisasa wa Ngelewala  uliokwama kwa miaka  tisa  sasa  katika Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa ambao unaohitaji  zaidi ya  shilingi bilioni 1.3  ili  kukamilika  kuchunguzwa na mkaguzi mkuu wa  hesabu za  serikali (CAG). Pamoja na  kuahidi  mradi  huo kuchunguzwa  ametaka  kupewa  BOQ za  mradi huo  ambao  amedai  kuwa una harufu ya ufisadi  na baadhi ya  wanasiasa  kukwamisha  kusudi   ili kupewa  kazi ya kuendesha mradi huo . Hapi  ametoa  agizo hilo  leo  wakati wa  ziara yake …

Soma Zaidi >>

KESI YA KUPINGA KUONDOLEWA CHANEL ZA NDANI KWENYE VISIMBUZI KUTAJWA OCTOBA 18

KESI  ya  kupinga  kuondolewa  kwa  chanel  za ndani  katika  visimbuzi vya Star Times , DSTV , Zuku   na  Azam  iliyopaswa kutajwa  Leo  katika mahakama  kuu kanda ya  Iringa imeahirishwa  hadi  Octoba 18  mwaka huu . Naibu  msajili  wa mahakama  kuu kanda ya  Iringa  Agatha  Chigulu ameihairisha   kesi  hiyo Leo  baada ya  jaji  aliyekuwa anasikiliza  kesi  hiyo   kuwa  kikazi  nje ya mahakama hiyo.  Katika   kesi   hiyo  namba 3 ya mwaka 2018 ilifunguliwa mahakamani hapo na watu watano Silvanus Kigomba Dr Jesca Msambatavangu, Oliver Motto,Sebastian  Atilio na Hamdun Abdallah  ilifunguliwa kwa jaji …

Soma Zaidi >>

DC ,SADA MALUNDE ATAKA SHERIA ZA MISITU KUONGEZWA MAKALI

  Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo Sada Malunde  amesema ni wakati umefika sasa kwa serikali kuangalia uwezekano wakurekebisha sheria za misitu na kuzifanya ziwe kali zaidi. Kuwa kuongezwa ukali kwa sheria za misitu kutasaidia kupunguza uharibifu wa hifadhi za misitu nchini unaofanywa kwa makusudi na watu wanaovamia misitu. Malunde ameyasema hayo alipotembelea msitu wa Nyantakara akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa lengo la kuona uvamizi na uharibifu unaoendelea katika hifadhi za misitu iliyopo wilayani humo. Katika ziara hiyo…

Soma Zaidi >>

UONGOZI SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA WAJIHAKIKISHIA KUENDELEA KUFANYA VIZURI MITIHANI

ZIKIWA zimepita siku  chache  toka wanafunzi  wa darasa la  saba nchini  kufanya  mtihani wa  Taifa wa darasa la saba  uongozi wa   shule ya  Southern Highlands Mafinga wilaya ya  Mufindi mkoani  Iringa  umewataka wazazi  kuanza  kuwaandaa watoto hao kujiunga na sekondari kwani ni  uhakika wa wanafunzi  hao kufaulu wote . Akizungumza  wakati wa  sherehe za  kuwaaga wanafunzi hao wa darasa la  saba shuleni hapo mkurugenzi mtendaji  wa  shule hiyo Bi  Mary Mungai ambae amepata  kuwa afisa  elimu wa  shule za msingi juzi alisema  sifa ya  shule hiyo ni kufanya  vizuri na…

Soma Zaidi >>

TUME YA HAKI ZA BINADAMU  IMEZITAKA WANACHAMA UN KUIWEKEA VIKWAZO BURUNDI

Geneva, USWIZI. Tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu Burundi imezitaka nchi wanachama kuendelea kuiwekea vikwazo nchi ya burundi na kuwalenga wahusika wa moja kwa moja na mauaji yanayotajwa katika ripoti ya tume hiyo. Tume hiyo imesema Jumuiya ya Kimataifa haikutekeleza jukumu lake ipasavyo ili kuingilia kati vilivyo kumaliza mzozo wa Burundi. Hayo yamejiri wakati tume hiyo ikiwasilisha ripoti yake mbele ya baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Jumatatu wiki hii huko Geneva Uswisi, ambapo wajumbe wa serikali ambao wapo mjini Geneva wamesusia…

Soma Zaidi >>

WATU 100 WAFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO NCHINI NIGERIA

Abuja, NIGERIA. Serikali ya Nigeria imetangaza hali ya maafa ya kitaifa baada ya mafuriko makubwa ambayo yamesababisha watu takribani mia moja kupoteza maisha. Mvua ya kubwa imesababisha mito ya Niger na Benue kujaa, na hivyo mafuriko kuyakumba maeneo wanakoishi watu, mashamba na kuwazuia maelfu ya watu katika nyumba zao. “Tumetangaza maafa ya kitaifa katika majimbo manne, jimbo la Kogi, Delta, Anambra pamoja na jimbo la Niger. Majimbo yote haya yameathiriwa na mafuriko. Watu wapatao 100 wamepoteza maisha katika majimbo 10,” amesema Sani Datti wa taasisi ya kitaifa kwa kukabiliana na…

Soma Zaidi >>