LIPUMBA AMUOMBA SEIF WAUNGANE

Ugunja, ZANZIBAR. Ikiwa ni siku chache tu zimepita toka kujiuzulu kwa mmoja wa viongozi wakuu Chama cha Wananchi (CUF),  ndugu Julius Mtatiro, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, ameibuka na kuomba mapatano kati yake na Katibu Mkuu wake Malim Seif Sharif Hamad. Prof. Lipumba ameyasema hayo katika mkutano wa ndani wa chama hicho uliowashirikisha baadhi ya viongozi toka upande wa Unguja ambapo amesema anaomba kumaliza tofauti zake na katibu mkuu Seif kwa ajili ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020. Lipumba amesema anatamani wanaposhiriki uchaguzi huo kuwepo na maelewano…

Soma Zaidi >>

AJIUZULU UDIWANI (CHADEMA) NA KUJIUNGA CCM, KAKONKO – KIGOMA

Diwani wa kata ya Katanga wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Osca Kazihise Bulakuvye, amejivua uanachama wake wa CHADEMA na hivyo kujihudhuru nafasi yake ya udiwani ndani ya kata hiyo. Bulakuvye amechukua maamuzi hayo hii leo ambapo tayari amemwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko kumtaarifu juu ya uamuzi wake huo. Katika barua yake, Bulakuvye ametaja sababu kuu ya kujiuzulu udiwani na kujiunga CCM kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania. Aidha, Bulakuvye amesema kuwa kilichomkimbiza kwenye chamachake cha zamani (CHADEMA) kuwa ni migogoro…

Soma Zaidi >>

MAGUFULI AENDELEA KUMMALIZA MBOWE, HAI DIWANI MMOJA ANG’OKA

Diwani wa kata Romu iliyopo Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Shilyimiaufoo mejiuzulu nafasi yake ya udiwani pamoja na kujivua uanachama wake wa Chadema na kujiunga chama cha Mapinduzi (CCM ). Kimaro amechukua maamuzi hayo hii leo ambapo tayari amemwandikia barua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Hai kumtaarifu juu ya uamuzi wake huo. Katika barua yake, Kimaro ametaja sababu kuu ya kujiuzulu udiwani na kujiunga CCM kuwa ni kukosekana kwa demokrasia ndani ya CHADEMA ambayo inaweza kuisaidia jamii katika kutatua matatizo na kuleta maendeleo na mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa…

Soma Zaidi >>

JESHI LA POLISI LATII AGIZO LA KUKAMATA WANAKIJIJI WOTE KIJIJI CHA NGOLE, MBEYA.

Tayari magari yaliyosheheni maaskari wa kutosha yametumwa katika Kijiji cha Ngole kilichopo kata ya Ilungu wilayani Mbeya kwaajili ya kuwakamata wanakijiji hao kutokana na kutuhumiwa kuharibu mradi wa maji katika kijiji jirani cha Msheye. Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyepo kijijini hapo amedai kuwepo kwa hofu kubwa miongoni mwa wananchi wa kijiji hicho. Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amenukuliwa na chombo kimoja cha habari nchini, akithibitisha kuwatuma askari wake kwaajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila. Mapema siku ya…

Soma Zaidi >>

RAIS TRUMP AAMURU AFISA USALAMA KUONDOLEWA ULINZI

Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru kuondolewa ulinzi aliyekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani ‘CIA’, John Brennan, kutokana na kile kinachodaiwa ni mtu asieaminika katika uadilifu na asiefuata misingi ya kazi yake katika siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa BBC, agizo la Trump limekuja ikiwa ni siku chache tu toka Brennan akaririwe akikosoa mkutano wa Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin uliofanyika mwezi Julai  katika mji wa Helsinki nchini Urusi. Brennan amepinga vikali agizo la Trump ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa hatua hiyo ni mwendelezo…

Soma Zaidi >>

MLIPUKO WA BOMU WAUA 48 NA KUJERUHI 67, WAKIWEMO WANAFUNZI WA CHUO KIKUU

Watu 48 wanaripotiwa kupoteza maisha huku wengine 68 wakijeruhiwa vibaya kufuatia mlipuko wa bomu uliotokea katika kituo kimoja cha masomo ya ziada mjini Kabul nchini Afghanstan. Tukio hilo limetokea mapema  jana ambapo polisi wamesema mwanamme mmoja aliyekuwa amejifunga mabomu hayo alifika katika kituo hicho cha elimu huko magharibi mwa Afghanstan na kujilipua katikati ya wanafunzi waliokuwepo eneo hilo. Kundi la wapiganaji wa Talban limekanusha kuhusika na shambulio hilo, licha ya kushutumiwa kutokana na kawaida yake ya kuwashambulia waumini wa Kishia ambao wengi wanapatikana katika eneo hilo ambapo washia  wanaonekana kama wapiganani…

Soma Zaidi >>