CHIRWA ANZAA KAZI AZAM FC ATUPIA DAKIKA YA 89

Na Shabani Rapwi, Dar es salaam. Mshambuliaji mpya wa klabu ya Azam FC, Obrey Chirwa alisajiliwa hivi karibuni kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nagoon FC ya Misri. Usiku wa leo Ijumaa ameanza rasmi kibarua chake ndani ya klabu hiyo,kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya Miaka 23 . Mchezo huo wakirafiki Azam FC wameibuka na ushindi wa magoli 2-0, goli la kwanza likifungwa na nyota Enock Atta dakika ya 12′ kwa mkwaju wa…

Soma Zaidi >>

BENKI KUU YA DUNIA YARIDHIA KUTOA BILIONI 680.5 KUBORESHA ELIMU YA SEKONDARI TANZANIA.

Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani Milioni 300 sawa na shilingi Bilioni 680.5 kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya sekondari unaokusudiwa kujenga vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, nyumba za watumishi na kununua vifaa vya kufundishia. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa inasema kuwa,Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Dkt. Hafez Ghanem aliyekutana na Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 16 Novemba, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam amesema pamoja na kuridhia kutoa…

Soma Zaidi >>

WATU SABA (7) WAUAWA NA JESHI LA POLISI MWANZA

Watu saba (7) wanaohofiwa kuwa ni majambazi wameuawa usiku wakuamkia leo katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi Maeneo ya Kishiri jijini Mwanza. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna, amesema jeshi la Polisu limefanikiwa kuwaua majambazi hao na kukamata silaha mbili za kivita na risasi zaidi ya 71. “Katika mapambano hayo yaliochukua zaidi ya Dakika 45 majambazi wote waliuawa na eneo la tukio tumekuta risasi zaidi ya 71 na silaha mbili za kivita.” Alieleza Kamanda Shanna. Kabla ya jeshi la polisi la…

Soma Zaidi >>

AZAM FC KURUDI TAIFA MECHI ZA SIMBA NA YANGA

Na Shaban Rapwi. Uongozi wa klabu ya Azam FC leo Novemba 16, 2018 umethibitisha uhamisho wa mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) ambazo watacheza dhidi ya Simba na Yanga kupigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari Msemaji wa klabu hiyo Jafar Idd Maganga amesema sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo ni kuwapa nafasi mashabiki wengi kushuhudia mechi hizo kutokana na Uwanja wa Azam Complex kuwa mdogo. Pia Jafar amesema licha ya udogo wa Uwanja changamoto walizopata kwenye mechi za kwanza zilizofanyika msimu…

Soma Zaidi >>

NIYONZIMA, DILUNGA KUMALIZA MCHEZO LEO

Na Shabani Rapwi, Dar es salaam. Klabu ya Simba SC yaweka hadharani kikosi kitakacho anza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Nyasa Bil Bullets, Haruna Niyonzima na Hassani Dilunga wakiongoza safu ya ushambuliaji, huku Wawa na Kaheza wakianzia bench. Ukiwa ni mchezo wa kirafiki utakao pigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Saa 12:00 Jioni. 1. Deogratias Munishi 2. Paul Bukaba 3. Mohamed Hussein 4. James kotei 5. Yusufu Mlipili 6. Said Ndemla 7. Mohamed Ibrahim 8. Mzamiru Yassin 9. Mohamed Rashid 10. Haruna Niyonzima 11. Hassan Dilunga…

Soma Zaidi >>

ORODHA YA MAWAZIRI NA WABUNGE WENYE MAHUDHURIO HAFIFU BUNGENI YATAJWA.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amewataja wabunge na mawaziri wenye mahudhurio hafifu zaidi katika vikao vya kamati za bunge na bungeni. Spika Ndugai,amewataja mawaziri hao na wabunge Leo bungeni jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi Cha maswali na majibu. Spika huyo amesema orodha hiyo inatokana na mahudhurio ya wabunge na mawaziri kwenye mkutano wa 11 kuanzia Bunge la Bajeti pamoja na mkutano wa 12. Mhe.Ndugai ametaja orodha ya mawaziri hao ni pamoja na Waziri Lukuvi (Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi) asilimia 40,…

Soma Zaidi >>

MTOTO WA MIAKA (8) ACHOMWA KISU BAADA YA KUVUNJA CHUPA.

Mtoto aliyefahamika kwa jina la Zainabu Hussein (8) amechumwa kisu na mama yake Ashura mkazi wa Tanga baada ya kuvunja chupa ya chai. Akisimulia tukio zima Mtoto Zainabu alisema kuwa kabla ya mama yake kuchomwa kisu kilichowekwa kwenye moto alichapwa viboko kwa sababu aliangusha chupa ya chai. “Siku ya Jumamosi mama Ashura alinichapa na kisha kunichoma na kisu ambacho alikuwa amekiweka kwenye moto kwa sababu nilikuwa nimebeba chupa ya chai kwa bahati mbaya ikaanguka na kupasuka ndiyo mama akanipiga halafu akachukua kisu na kukiweka kwenye moto kisha akaanza kunichoma nacho…

Soma Zaidi >>

SUBIRA MGALU AKUTANA NA UBALOZI WA AUSTRIA WAJADILI JUU YA KUWEKEZA KWENYE NISHATI NA SEKTA NYINGINE MWAKANI.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya mazungumzo na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Austria, Kurt Mullauer wenye ofisi zake Nairobi-Kenya (sehemu ya biashara). Kurt Mullauer alifika wizarani hapo kwa lengo la kumweleza Mh. Subira Mgalu kuhusu Ujumbe wa Kibiashara kutoka Austria unaotarajiwa kuwasili nchini mwezi Januari, 2019. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Eng.Innocent Luoga na Mwakilishi wa Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Ebenezer Mollel. Kurt Mullauer amemweleza Naibu Waziri kuwa, ujumbe huo wa…

Soma Zaidi >>

MDAMI: BILA KITAMBULISHO CHA TAIFA HUWEZI KUPATA HUDUMA YEYOTE NCHINI.

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), imesema kuwa huduma nyingi kwa sasa zinategemea vitambulisho vya taifa na hayo yanafanyika ili kuongeza msukumo wa watu kufatilia vitambulisho hivyo. Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio msemaji wa NIDA, Rose Mdami amesema kuwa mamlaka hiyo inataka kila mtu mwenye umri wa miaka 18 awe na kitambulisho, kwani matumizi yataongezeka zaidi ya hapo. “Mpaka sasa tumeshaandikisha wananchi milioni 19, na lengo tufike zaidi ya hapo na adhma yetu kila Mtanzania awe na kitambulisho cha taifa ili iwe rahisi kutambuana,…

Soma Zaidi >>

DIWANI WA VITI MAALUM MANISPAA YA ILALA NEEMA NYANGALILO ATEMBELEA YATIMA.

Na Heri Shaaban. Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangalilo amesherekea miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Magufuli kwa kugawa vyakula katika kituo cha watoto Yatima Msimbazi wilayani Ilala. Katika hafla hiyo ya kutembelea watoto yatima wa Msimbazi Diwani Neema aliongozana Umoja wa Wanawake wa( UWT) kata ya Ilala. “Mimi kama Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala nimpongeza Rais wangu Magufuli katika uongozi wake pia nimetumia siku ya leo kushiriki katika kituo cha Msimbazi kuwaona watoto na kuwapa misaada”alisema Neema. Neema alisema msafara wake alikuwa…

Soma Zaidi >>