MTATIRO: SIJAPANGA MIPANGO YA KUHAMIA CCM WALA SINA NIA HIYO

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, ametolea ufafanuzi madai ya yeye kuhamia CCM. Mtatiro alisema, anapenda kuujulisha Umma kuwa, ameona propaganda nyingi kwenye mitandao juu ya yeye kuhamia CCM au kuwa na mipango ya kuhamia CCM. “Nataka niwahakikishie watanzania kuwa sijapanga mipango hiyo na sina nia hiyo, na naomba niwajulishe kuwa mtu akiwa anahamia CCM, hamuwezi kuwa na tetesi in advance – hutokea tu “PAAAP” – na mimi sina kawaida ya kufanya maamuzi ghafla na kwa kujificha,”alisema Mtatiro. Alisema,  angelikuwa na nia ya kuhamia CCM angewataarifu…

Soma Zaidi >>

TAARIFA FUPI KWA UMMA. Ndugu zangu, nimeona PROPAGANDA nyingi kwenye mitandao juu ya mimi kuhamia CCM au kuwa na mipango ya kuhamia CCM. Nataka niwahakikishie watanzania kuwa SIJAPANGA mipango hiyo na sina nia hiyo. Na naomba niwajulishe kuwa mtu akiwa anahamia CCM, hamuwezi kuwa na tetesi in advance – hutokea tu “PAAAP” – na mimi sina kawaida ya kufanya maamuzi ghafla na kwa kujificha. Ningelikuwa na nia ya kuhamia CCM ningewataarifu hapa hadharani, miezi kadhaa kabla ya kufanya hivyo, walau jambo moja ambalo Mungu alinijalia ni kutokuwa MWOGA na MNAFIKI…

Soma Zaidi >>

SAED KUBENEA: SIWEZI KUHAMA CHADEMA KWENDA CCM, MWENYE USHAHIDI AUTOE

Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Saed Kubenea, amekanusha madai yanayoenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa anampango wa kukihama chama hicho na kwenda CCM. Mbunge huyo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa maneno ya chini chini kuwa, anataka kukihama chama hicho kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wabunge wa upinzani waliamua kuondoka katika vyama vyao kwa madai ya kwenda kuunga mkono jitihada za utendaji wa Rais Magufuli. Alisema, anatarajia kuongea na Vyombo vya…

Soma Zaidi >>

POLISI ZANZIBAR YAENDELEA KUMSHIKILIA MFANYABIASHARA ALIYEKUTWA NA DHAHABU NA FEDHA ZA NCHI 15

Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, Ramadhan Ng’azi alisema kuwa,  Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia mfanyabiashara aliyekamatwa na dhahabu na Mamilioni ya fedha za nchi  15 mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika. Mkurugenzi huyo alisema, juhudi za kukamilisha uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa huyo bado zinaendelea na kwamba sio rahisi kutoa taarifa kwa umma kuwa ni wapi wamefikia katika uchunguzi huo. “Hatuwezi kusema tumefikia wapi hadi pale tutakapokamilisha kazi yetu ila tunaendelea kumshikilia kwa mujibu wa taratibu zetu,” alisema Ng’azi. Kwa uapande wake kaimu Kamishna wa Polisi Zanzibar Juma Yusuph Ali, alisema…

Soma Zaidi >>

WANAFUNZI 225 KUSHIRIKI GWARIDE LA MKOLONI MIAKA 50 YA UHURU

Jumla ya watoto 225 kutoka Shule mbali mbali za Sekondari nchini, wanatarajia kushiriki katika Gwaride Maalum la Mkoloni litakalofanywa na Jeshi la Polisi katika kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Dodoma Desemba 9, mwaka huu. Akizungumzia maandalizi ya sherehe hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge alisema kuwa, lengo la kuwashirikisha watoto hao ni kuwafundisha na kuwarithisha tunu ya Uhuru , Uzalendo, Umoja na Mshikamano wa Taifa lao. Alisema, hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa gwaride la mkoloni kufanyika katika sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi anatarajiwa…

Soma Zaidi >>

TRUMP KUTANGAZA RASMI KUUTAMBUA MJI WA JERUSALEM NA KUHAMISHIA UBALOZI WAKE

 Rais wa marekani Donald Trump anatarajia kuutangazia Ulimwengu kuwa, wanautambua Mji wa Jerusalem kama mji Mkuu wa Israel na hivyo kuhamishia Ubalozi wake rasmi ambao awali ulikuwa katika mji wa Tel Aviv. Imeelezwa kuwa, uamuzi huo wa rais Trump umethibitishwa na Ikulu ya White House ambapo Rais Trump atazungumza leo kuhusu juu ya kutangaza rasmi kuhamishiwa kwa ubalozi wa Marekani Jerusalem. Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Marekani White house, Sarah Sanders amesema kuwa, Trump alizungumza na baadhi ya viongozi siku ya Jumanne kuhusu mpango wake wa kuhamishia ubalozi…

Soma Zaidi >>

MAJAMBAZI WATATU WAUAWA AKIWEMO “KOMANDOO” KUTOKA BURUNDI

Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam imetoa taarifa kuhusiana na kuuawa kwa majambazi watatu akiwemo Mrundi mmoja “Komandoo” na kupatikana na silaha moja ya kivita aina ya AK 47 na risasi 57. Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa makosa yaliyotokea katika kipindi cha wiki mbili zilizopita na kwamba Novemba 28 na 30, mwaka huu askari walifanya oparesheni maalum ambayo ilifanikisha kukamatwa na watuhumiwa watatu ambao walidaiwa kulihusika na unyang’anyi wa kutumia silaha na kufanya mauaji  katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Saalaam. Kamanda Mambosasa alisema,…

Soma Zaidi >>

Na Alex Massaba Mwenyekiti Wa Baraza la Vijana Wa Chadema taifa (Bavicha) Kamanda Patrick Ole Sosopi leo tarehe 05/12/2017 amemtembelea Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Ilala Mhe. Charles Kuyeko Ofisini kwake maeneo ya Mnazi mmoja…Anatoglou. Viongozi hao wawili wamebadilishana mawazo ya kiongozi hususani nafasi ya vijana katika Manispaa tunazoziongoza. Ziara hiyo ya Mwenyekiti Wa Bavicha taifa ni moja ya mipango ya utendaji kazi aliyoipanga ya kutembelea Halimashauri na Manispaa zote zinazoongozwa na Mameya na Wenyeviti Wa Chadema nchi nzima. Lengo kuu la ziara hiyo ni kujadili fursa zilizopo kwenye Halmshauri…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI AKEMEA WASANII KUTUMIA MITANDAO KUJIDHALILISHA

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Juliana Shonza amekemea tabia ya Wasanii kutumia vibaya mitandao kwa kujidhalilisha badala ya kutumia kwa kutuletea maendeleo. Mhe.Shonza aliyasema hayo hii leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo Tanzania ambapo aliongea na wasasii mbali mbali ambao ndio waendeshaji wa kampeni hiyo. Alisema, haipendezi kuona msanii anatumia vibaya mitandao kwa kuposti picha za kujidhalilisha na kumdhalilisha mwanamke na kwamba lengo la kuletwa kwa mitandao hii ni kusaidia kurahisisha mawasiliano na kuleta maendeleo kwa taifa. “Msanii ni kioo cha jamii na nyie…

Soma Zaidi >>

LIJUALIKALI, SUZAN NA WENZAO 36 WA CHADEMA WARUDISHWA RUMANDE MOROGORO

Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, imeamuru Wabunge Susan Kiwanga na Peter Lijualikali na wenzao 36, warudishwa rumande kufuatia kuibuka mvutano kuhusiana na hati ya kiapo kupinga dhamana iliyowasilishwa na upande wa mashtaka mahakamani hapo. Awali mahakama hiyo ilipanga kutoa uamuzi wa washtakiwa kupata au kutokupata dhamana hii leo ambapo hata hivyo Hakimu Ivan Msack aliahirisha kesi hiyo hadi hapo kesho Jumatano, Desemba 6,2017 ili kutoa nafasi kwa pande zote mbili ya utetezi na upande wa mashtaka kujibu hoja kuhusiana na hati hiyo. Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo…

Soma Zaidi >>