KUSUASUA KWA MIRADI YA MAJI KYERWA NAIBU WAZIRI AAGIZA MKANDARASI KUONDOLEWA

Na mwandishi wetu-Kagera. Kufatia kusuasua kwa miradi ya maji wilayani Kyerwa na kushindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi wilayani humo,Naibu waziri wa maji Mhe.Jumaa Aweso amemuagiza mhandisi wa maji mkoa wa Kagera kumsimamisha kazi mkandarasi anayetekeleza miradi ya maji wilayani Kyerwa kutokana na kutokuwa na uwezo pamoja na vigezo. Naibu waziri ametoa agizo hilo januari 12 mwaka huu akiwa ziarani katika wilaya za Karagwe na Kyerwa ambapo imeonekena miradi mingi ya maji katika wilaya hizo ni kutokana na makandarasi wanaopewa kazi ya kujenga miradi hiyo kutokuwa na uwezo. Aweso…

Soma Zaidi >>

HIKI NDICHO KINACHOMUUMIZA KICHWA WAZIRI LUGOLA KATIKA WIZARA YAKE.

  Na Allawi Kaboyo Bukoba. WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola,amesema kitu kinachomuumiza kichwa katika wizara yake ni Idara ya huduma za uangalizi na probesheni licha ya kuwa na watumshi wengi katika wizara hiyo. Alitoa kauli hiyo Jana wakati akipokea taarifa za idara hiyo Mkoani Kagera ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake mkoani humo kwa muda wa siku saba atakaoumaliza. Waziri Lugola,alisema watumishi wa wizara hiyo wizarani ni 160 lakini shughuli zake hazifahamiki kwa jamii. Alisema kwa hali ilivyo Wizara inamzigo wa kuibeba idara hiyo…

Soma Zaidi >>

DKT.BASHIRU “MKUU WA MKOA ATAKAYESHINDWA KUSIMAMIA HAKI ZA BODABODA NA MACHINGA HANA KAZI”

Na Allawi Kaboyo-Bukoba. Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi  CCM Daktari Bashiru Ally Kakurwa, amewataka watendaji wa Serikali hususani wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini,  kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa haki wakati wa kuwatumikia Wananchi wao pasipo kulegalega. Kauli hiyo ameitoa desemba 22 mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchama wa chama hicho waliojitokeza kumlaki alipowasili mkoani Kagera na kumtolea mfano Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kwa Nidhamu, Uzalendo, Ujasiri na Uchapakazi wake uliotukuka aliouonyesha kwa Kipindi Kifupi toka Ameteuliwa. “Niwaombe wananchi wa mkoa wa…

Soma Zaidi >>

WAKURUGENZI WA SERA NA MIPANGO NA MAAFISA UTUMISHI WAANDAMIZI WAJENGEWA UWEZO WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU

Na; Mwandishi Wetu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na SHIVYAWATA wametoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakurugenzi wa Sera na Mipango na Maafisa Utumishi Waandamizi juu ya masuala ya Watu wenye Ulemavu. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Peter Kalonga amesema kuwa masuala ya Watu wenye Ulemavu ni mtambuka, hivyo ili kuifikia jamii jumuishi ni vyema kuhakikisha masuala ya wenye Ulemavu yanajumuishwa vyema katika mipango mkakati wa…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA AWAMU YATANO IMEKUSUDIA KUIMARISHA SEKTA YA NISHATI NCHINI.

Na mwandishi wetu Songea. Naibu waziri wa nishati ,Mheshimiwa Subira Mgalu amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano chini ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuimarisha sekta ya Nishati Nchini kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kuhakikisha Nchi inakua na Umeme wa Uhakika , na hilo limethibitika kwa kuanza mchakato wa ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya mto Rufuji mkoani Njombe utakaozalisha megawats 358 kwa lengo la kuwa na umeme wa kutosha na wa gharama nafuu. Akizungumza na wananchi wakati akiwasha umeme…

Soma Zaidi >>

RC KAGERA “WATAKAOHUJUMU ZOEZI LA VITAMBURISHO KUKIONA CHA MOTO”

Na: Mwandishi wetu Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti atekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli la kugawa vitambulisho kwa Wajasiliamli Wadogo ili waweze kufanya shughuli zao za ujasiliamali na kujiingizia kipato chao cha kila siku bila kusumbuliwa na mtu yeyote. Mhe.Gaguti ametekeleza agizo hilo la Rais Magufuli Desemba 20, 2018 katika Uwanja wa Uhuru (Maarufu kama Mayunga) Manispaa ya Bukoba ambapo amevigawa vitambulisho hivyo kwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Kagera na Halmashauri zake nane.…

Soma Zaidi >>

WAKAZI WA MANISPAA NA MIJI KUNUFAIKA NA UMEME WA REA

  Na Mwandishi wetu Ruvuma. Shirika la umeme nchini Tanesco mkoani Ruvuma kupitia wakala wa kusambaza umeme vijijini Rea limeendelea kusambaza umeme katika vijiji mbalimbali vilivyopo kwenye mpango ndani ya mkoa wa Ruvuma na kuwafanya wananchi mkoani humo kunufaika na matunda ya serikali ya awamu ya tano. Akitoa salamu za shukrani kwa uongozi wa Tanesco mkoa wa Ruvuma kutokana na kasi waliyonayo ya kuhakikisha wananchi mkoani humo wanapata nishati hiyo, Mhe Subira Mgalu, Naibu Waziri Nishati amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Namis kufanya kazi kwa kasi na umakini ili kuondoa…

Soma Zaidi >>

MKANDARASI ATAKAYE SUASUA KATIKA SUALA LA UMEME KUNYANGANYWA KAZI

  Na Mwandishi wetu Ruvuma. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu ameendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi ya umeme mkoani Ruvuma ambapo leo amewasha umeme Kijiji cha Palangu na Mang’ua pamoja mtaa wa Luhila Seko katika Wilaya ya Songea ambavyo vimepata umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) mzunguko wa kwanza na mradi wa Makambako – Songea. Huo ni muendelezo wa kazi ya ukaguzi na uzinduzi wa miradi ya umeme vijijini mkoani Ruvuma aliyoianza tarehe17 Disemba, 2018 kwa kuwasha umeme katika Vijiji…

Soma Zaidi >>

AUMUUA KIKATILI HAWALA YAKE KISHA NA YEYE KUJIUA

Na Allawi Kaboyo Bukoba. Watu wawili wanaodaiwa walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi wamefariki baada mmoja kunyongwa na mwingine kujinyonga, katika mtaa wa Mafumbo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera. Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi alisema kuwa mauaji hayo yamegundulika Desemba 17 mwaka huu saa 11 jioni katika mtaa huo. Malimi alimtaja anayedaiwa kunyongwa na mpenzi wake kuwa ni Regina Temu (29) mkazi wa Kahororo pia katika manispaa hiyo, na mfanyakazi wa kiwanda cha kusindika kahawa cha Tanica, aliyekutwa amenyongwa kwa tai. Alisema kuwa baada ya huyo mpenzi wake…

Soma Zaidi >>