ANATAKA UMAARUFU KUPITIA MIMI WALA SIKUMBAKA: RONALDO

Na Jyross Curtis

Mchezaji bora na ghari duniani katika dimbwi la soka, Cristiano Ronaldo, amekana madai ya mwanadada Kathryn Mayorga alietoa madai ya kubakwa na Ronaldo mnamo mwaka 2009 katika moja ya hoteli jijini Las Vegas, Marekani.

Staa huyo wa kandanda alionekana katika video yake ya Instagram akikataa madai ya mwanamke huyo kwa kusema “Wanataka umaaruufu kupitia jina langu, ni kawaida yao”.

Hata hivyo mawakili wa Ronaldo nao hawakupendezwa na taarifa hiyo iliyotolewa kupitia jarida la ujerumani la Der Spiegel na hivyo basi wameamua kulishitaki kwa kuripoti madai hayo ysiyo ya ukweli kutokana kwa mwanamke huyo.

Bi. Kathryn Mayorga anaripotiwa kuwa kaandika madai hayo kwa polisi wa jiji la Las Vegas muda mfupi baada ya kutoa madai hayo, pia ameripoti kuwa baada ya kubakwa, aliingia mkataba wa dola 375,000 na Ronaldo ili kuificha siri hiyo.

Ronaldo akiwa katika kupinga madai hayo, mawakili wa Kathryn wanahimiza kesi kusikilizwa na huku mawakili wa Ronaldo wakitaka makubaliano ya madai hayo kutupiliwa mbali kabisa.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.