AJIUZULU UDIWANI (CHADEMA) NA KUJIUNGA CCM, KAKONKO – KIGOMA

Diwani wa kata ya Katanga wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Osca Kazihise Bulakuvye, amejivua uanachama wake wa CHADEMA na hivyo kujihudhuru nafasi yake ya udiwani ndani ya kata hiyo.

Bulakuvye amechukua maamuzi hayo hii leo ambapo tayari amemwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko kumtaarifu juu ya uamuzi wake huo.

Katika barua yake, Bulakuvye ametaja sababu kuu ya kujiuzulu udiwani na kujiunga CCM kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

Aidha, Bulakuvye amesema kuwa kilichomkimbiza kwenye chamachake cha zamani (CHADEMA) kuwa ni migogoro isiyoisha ndani ya chama hicho ambayo haiisaidii jamii katika kujiletea maendeleo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.