CHIRWA ANZAA KAZI AZAM FC ATUPIA DAKIKA YA 89

Na Shabani Rapwi, Dar es salaam. Mshambuliaji mpya wa klabu ya Azam FC, Obrey Chirwa alisajiliwa hivi karibuni kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na klabu ya Nagoon FC ya Misri. Usiku wa leo Ijumaa ameanza rasmi kibarua chake ndani ya klabu hiyo,kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania chini ya Miaka 23 . Mchezo huo wakirafiki Azam FC wameibuka na ushindi wa magoli 2-0, goli la kwanza likifungwa na nyota Enock Atta dakika ya 12′ kwa mkwaju wa…

Soma Zaidi >>

RC MAKONDA ATEMBELEA STAND YA MABASI MSAVU MOROGORO.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiwa ameambatana na Mstahiki Meya wa jiji, Mamea wa Halmashauri na Madiwani wamefanya ziara Mkoani Morogoro kwenye kituo kipya cha Mabasi  Msamvu kujifunza namna kituo hiko cha mabasi kimefanikiwa kuweka mazingira jumuishi kwa makundi yote wakiwemo wafanyabiashara na wasafiri. Mkuu wa mkoa Makonda amesema Dar es salaam ipo katika hatua ya ujenzi wa kituo kipya cha Mabasi cha kisasa Mbezi Luis itakayogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 50.9 ambayo itakuwa na ukubwa mara nne ya kituo cha Msamvu ambapo kitakuwa…

Soma Zaidi >>

MKUU WA WILAYA YA KILINDI AKUTANA NA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO NA KUTEMBELEA MRADI WA REA.

  Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mheshimiwa Sauda Mtondoo hii leo ametembelea wafanyabiashara ndogo ndogo na kukagua mradi wa umeme wa REA. Mhe. Sauda ameongozana na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Makasini kupita kwa wafanyabiashara ndogo ndogo eneo la Kwediboma kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitolea ufumbuzi. Sambamba na kusikiliza kero za wafanyabiashara ndogo ndogo Mhe. Mkuu wa Wilaya aliweza kukagua mradi wa umeme wa REA uliopo Kijiji Cha Gombero katika kuhakikisha maagizo ya Waziri wa Nishati Mhe. Merdad Kalemani yametekelezwa tangu alipofanya ziara wilayani humo mnamo…

Soma Zaidi >>

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI BABATI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameutaka Uongozi wa mkoa wa Manyara kutumia sheria za mazingira kulinda vyanzo vya maji. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo mjini Babati akiwa kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo. “Tumieni sheria ya mazingira inayotaka kuwe na mita 60, hii itasaidia kulinda na kutunza vyanzo vya maji, washirikisheni wataalam wa mazingira katika hili” alisema Makamu wa Rais. Leo katika ziara yake wilayani Babati, Makamu wa Rais ametembelea kiwanda cha mbolea Minjingu, amezindua jengo la Ofisi…

Soma Zaidi >>

BENKI KUU YA DUNIA YARIDHIA KUTOA BILIONI 680.5 KUBORESHA ELIMU YA SEKONDARI TANZANIA.

Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani Milioni 300 sawa na shilingi Bilioni 680.5 kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya sekondari unaokusudiwa kujenga vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, nyumba za watumishi na kununua vifaa vya kufundishia. Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Gerson Msigwa inasema kuwa,Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Dkt. Hafez Ghanem aliyekutana na Mhe. Rais Magufuli leo tarehe 16 Novemba, 2018 Ikulu Jijini Dar es Salaam amesema pamoja na kuridhia kutoa…

Soma Zaidi >>

WATU SABA (7) WAUAWA NA JESHI LA POLISI MWANZA

Watu saba (7) wanaohofiwa kuwa ni majambazi wameuawa usiku wakuamkia leo katika majibizano ya risasi na Jeshi la Polisi Maeneo ya Kishiri jijini Mwanza. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna, amesema jeshi la Polisu limefanikiwa kuwaua majambazi hao na kukamata silaha mbili za kivita na risasi zaidi ya 71. “Katika mapambano hayo yaliochukua zaidi ya Dakika 45 majambazi wote waliuawa na eneo la tukio tumekuta risasi zaidi ya 71 na silaha mbili za kivita.” Alieleza Kamanda Shanna. Kabla ya jeshi la polisi la…

Soma Zaidi >>

AZAM FC KURUDI TAIFA MECHI ZA SIMBA NA YANGA

Na Shaban Rapwi. Uongozi wa klabu ya Azam FC leo Novemba 16, 2018 umethibitisha uhamisho wa mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) ambazo watacheza dhidi ya Simba na Yanga kupigwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari Msemaji wa klabu hiyo Jafar Idd Maganga amesema sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo ni kuwapa nafasi mashabiki wengi kushuhudia mechi hizo kutokana na Uwanja wa Azam Complex kuwa mdogo. Pia Jafar amesema licha ya udogo wa Uwanja changamoto walizopata kwenye mechi za kwanza zilizofanyika msimu…

Soma Zaidi >>

NIYONZIMA, DILUNGA KUMALIZA MCHEZO LEO

Na Shabani Rapwi, Dar es salaam. Klabu ya Simba SC yaweka hadharani kikosi kitakacho anza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Nyasa Bil Bullets, Haruna Niyonzima na Hassani Dilunga wakiongoza safu ya ushambuliaji, huku Wawa na Kaheza wakianzia bench. Ukiwa ni mchezo wa kirafiki utakao pigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Saa 12:00 Jioni. 1. Deogratias Munishi 2. Paul Bukaba 3. Mohamed Hussein 4. James kotei 5. Yusufu Mlipili 6. Said Ndemla 7. Mohamed Ibrahim 8. Mzamiru Yassin 9. Mohamed Rashid 10. Haruna Niyonzima 11. Hassan Dilunga…

Soma Zaidi >>

MEYA MANISPAA YA IRINGA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Na Francis Godwin,Iringa TAASISI  ya  kuzuia na kupambana na Rushwa  nchini (TAKUKURU) imemfikisha   mahakamani mstakihi   meya  wa  halmashauri ya  manispaa ya  Iringa Alex  Kimbe kupitia  chama  cha  demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)   makosa  mawili  ya  jinai kuomba na  kupokea  rushwa . Kaimu  kamanda  wa  takukuru  mkoa  wa  Iringa  Mweli Kilimali   akizungumza leo na  vyombo  vya habari  ofisibni  kwake  alisema kuwa   meya  huyo alipokea kiasi cha  shilingi  milioni 2  kutoka kwa  mteja  wao . Alisema  kuwa  tukio  la kukamatwa meya  huyo lilitokea  Novemba  15  mwaka  huu majira ya saa 12  jioni …

Soma Zaidi >>

AFISA KILIMO MSTAAFU APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUSABABISHA KIFO CHA MWENYEKITI UWT.

Na Dinna Maningo,Tarime. JESHI la polisi Tarime/ Rorya limemfikisha katika Mahakama ya wilaya ya Tarime Afisa kilimo mstaafu Wilayani Rorya Salala  Nyakiriga (67) kwa makosa matatu ya kusababisha kifo,Kujeruhi na kuendesha gari akiwa amelewa. Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Tarime Veronica Mugendi,Mwendesha mashitaka wa Polisi Saumu Ngoma alisema kuwa Mtuhumiwa huyo Novemba 13,2018 majira ya saa moja jioni akiwa anaendesha  Gari aina ya Toyota  lenye namba za usajili T 264 DLA,ambaye ni mkazi wa Obwere wilayani Rorya alimgonga Mwenyekiti wa umoja wa wanawake(UWT) chama cha Mapinduzi (CCM)…

Soma Zaidi >>