MDAMI: BILA KITAMBULISHO CHA TAIFA HUWEZI KUPATA HUDUMA YEYOTE NCHINI.

Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA), imesema kuwa huduma nyingi kwa sasa zinategemea vitambulisho vya taifa na hayo yanafanyika ili kuongeza msukumo wa watu kufatilia vitambulisho hivyo. Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast cha East Africa Radio msemaji wa NIDA, Rose Mdami amesema kuwa mamlaka hiyo inataka kila mtu mwenye umri wa miaka 18 awe na kitambulisho, kwani matumizi yataongezeka zaidi ya hapo. “Mpaka sasa tumeshaandikisha wananchi milioni 19, na lengo tufike zaidi ya hapo na adhma yetu kila Mtanzania awe na kitambulisho cha taifa ili iwe rahisi kutambuana,…

Soma Zaidi >>

DIWANI WA VITI MAALUM MANISPAA YA ILALA NEEMA NYANGALILO ATEMBELEA YATIMA.

Na Heri Shaaban. Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangalilo amesherekea miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Magufuli kwa kugawa vyakula katika kituo cha watoto Yatima Msimbazi wilayani Ilala. Katika hafla hiyo ya kutembelea watoto yatima wa Msimbazi Diwani Neema aliongozana Umoja wa Wanawake wa( UWT) kata ya Ilala. “Mimi kama Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala nimpongeza Rais wangu Magufuli katika uongozi wake pia nimetumia siku ya leo kushiriki katika kituo cha Msimbazi kuwaona watoto na kuwapa misaada”alisema Neema. Neema alisema msafara wake alikuwa…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI ATOA MAAMUZI MAGUMU UNUNUZI WA KOROSHO ZOTE ZA WAKULIMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Novemba, 2018 ametangaza uamuzi wa Serikali kununua korosho zote za wakulima msimu huu kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo baada ya wanunuzi binafsi kushindwa kutimiza maagizo ya Serikali kwa kuanza kununua kwa kusuasua na kwa bei isiyoridhisha. Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph George Kakunda, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga, Naibu Waziri Ofisi…

Soma Zaidi >>

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI SAME NA MWANGA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Maendeleo pasipo Utawala bora. Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro. “Viongozi wa Halmashauri, Viongozi wa Wilaya wasipokuwa na Utawala bora, wasiposhirikiana, Chama, Serikali, Wilaya, Halmashauri tusitegemee kuwa na maendeleo tutalalamika siku zote” alisema Makamu wa Rais. Leo katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo Makamu wa Rais alitembelea miradi mbali mbali katika Wilaya ya Same na Mwanga. Akiwa Wilayani Same, Makamu…

Soma Zaidi >>

BASATA YAUFUNGIA WIMBO MPYA WA RAYVANNY NA DIAMOND…WCB WASEMA HAWANA TAARIFA.

Wakati Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Kitomali wakikosa dhamana tena hii leo baada ya wadhamini wao kutofika kwenye kesi inayowakabili katika Mahakama ya Kisutu Dar es salaam ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, Maneno “michezo ya Amber Ruty” yawaponza Diamond na Rayvanny. Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii. Mtandao wa DarMpya umezungumza na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, na amethibitisha kuwa leo Jumatatu Novemba 12,2018 kuwa wameufungia wimbo huo ambao…

Soma Zaidi >>

WAZIRI KALEMANI AIVUNJA BODI YA (REA)

Na Jasmine Shamwepu,Dodoma. Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameivunja rasmi Bodi ya wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutokana na kutoridhishwa na utendaji wake. Sambamba na hilo,Waziri Kalemani ametengua rasmi nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Gideon Kaonda pamoja na wajumbe saba waliyokuwa kwenye Bodi ya REA. Uamuzi huo wa kuivunja bodi ya wakurugenzi wa REA ameutoa leo Ofisini kwake Jijijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Amesema kuwa, bodi hiyo iliundwa rasmi mwaka jana kwa mujibu wa sheria ya wakala vijijini namba 8 ya…

Soma Zaidi >>