MADIWANI WA CCM IRINGA MJINI WASUSA BARAZA LA MADIWANI

Na Francis Godwin, Iringa KIKAO   cha  baraza la madiwani  wa halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  kimeshindwa  kufanyika  baada ya madiwani wa   chama  cha mapinduzi (CCM)  kususia kikao hicho   wakipinga  kile  walichodai ni ubabe wa mstahiki meya  kupitia  chama  cha Demokrasia na maendeleo  (CHADEMA) Alex  Kimbe katika  uundaji wa kamati mbali mbali na uendeshaji wa vikao hivyo. Akizunguza leo  na waandishi  wa habari katika   ofisi ya  CCM wilaya ya Iringa mjini naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Joseph Lyata  alisema kuwa  uamuzi wa  kutoingia katika  kikao  hicho   ni kutokana na…

Soma Zaidi >>

MSIGWA AIBUKA BUNGENI NA SAKATA LA MO DEWJI KUTEKWA

Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), ameibua suala la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji kiaina. Akichangia mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka 2019/20 bungeni leo Jumanne Novemba 6, 2018 , Mchungaji Msigwa alisema wafanyabiashara hawako huru kufanya biashara nchini. “Wawekezaji wanajionaje kuwepo katika nchi hii, wapo salama? Takwimu zinaonyesha wawekezaji wa nje wanafunga virago. “Je wawekezaji wa ndani wakoje? Wana raha? Kama bilionea mkubwa nchi hii anaweza akashikwa, akafichwa, akaachiwa halafu hadi leo hajaruhusiwa kusema alikuwa wapi unadhani nani atakuja kuweka biashara hapa ndani? Haya…

Soma Zaidi >>