NAIBU WAZIRI JOSEPH KAKUNDA AZITAKA HALMASHAURI KWENDA KUJIFUNZA KIBITI.

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Joseph Kakunda leo October 20 2018 amejionea vyumba 7 vya madarasa na ofisi mbili katika shule ya Mtawanya wilayani Kibiti ambapo ujenzi wake uligharimu milion 66.6 amesema ni kitu cha mfano na kuzitaka halmashauri zote kwenda wakajifunze kwenye shule hiyo. Kakunda amebainisha hayo akisema “Kilichofanyika kwenye Shule ya msingi Mtawanya wilayani Kibiti ni kitu cha mfano kinachopaswa kuigwa na halmashauri nyingine nchini. Serikali iliwapatia milioni 66.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa badala yake wamejenga vyumba 7 na ofisi mbili.…

Soma Zaidi >>

TARESO YAWATAKA WANATAALUMA WA KUMBUKUMBU KUJIUNGA NA CHAMA HICHO

  Dar es Salaam Chama cha wataalam watunzaji wa kumbukumbu Tanzania (TARESO) kimewataka wafanyakazi wenye taaluma ya utunzaji kumbukumbu nchini kujitokeza kwa wingi kujiunga ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja. Kauli hiyo imetolewa mapema leo jijini Dar es Salaam na Afisa Mtunzaji kumbukumbu Mwandamizi (Brela) Mwombeki Rutta, wakati alipokua katika kikao cha kupitisha rasimu ya katiba ya chama hicho. Amesema kuwa, Chama hicho kimekuwa kikifanya kazi nchi nzima kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu, madaktari pamoja na wabobezi wa tasnia hiyo. “Chama hiki ni…

Soma Zaidi >>

NAIBU MSAJILI WA MAHAKAMA AWATAKA MAHAKIMU KUZINGATIA MAADILI

  Dar es Salaam Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Joachim Tiganga, amewataka mahakimu kuzingatia maadili katika utoaji haki ili kulinda heshima yao wenyewe na kuwajengea wananchi imani juu ya mhimili huo. Kauli hiyo jijini Dar es Salaam mapema wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo mahakimu wanawake wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusu maadili ya viongozi wa umma yaliyoendeshwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Amesema kuwa, ikiwa mahakimu hawatatenda haki katika maamuzi wanayoyafanya watasababisha watu kujichukulia sheria mkononi hali…

Soma Zaidi >>

KAMPENI YA FURAHA YANGU WILAYANI NAMTUMBO YAZIDI KUCHANJA MBUGA.

    Namtumbo Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mheshimiwa Sophia Mfaume ameendelea na kampeni ya furaha yangu kwa kufungua mashindano ya mpira wa miguu wilayani humo. Aidha amesema kuwa, wilaya hiyo,wameendeleza jitihada zao kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu iitwayo Laiganani super cup ambapo maana ya jina hilo ni neno la kimasai linalohamasisha vijana. “Tumeendeleza jitihada hizi kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu ambapo lengo ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaokutwa na VVU kuanza dozi mapema ” amesema DC Kizigo Aidha amesema, lengo…

Soma Zaidi >>

IGP SIMONI SIRRO AWAONYA WANAOTAKA KULIFUNDISHA KAZI JESHI LA POLISI.

    Dar es Salaam Kamanda Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro leo tarehe oktoba 20, 2018 amekutana na kuzungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuzungumzia juu ya tukio la kupatikana kwa Mfanyabishara Mohamed Dewji. Akizungumza na vyombo vya habari IGP Simon Sirro amesema “Nyinyi ni mashahidi jana nimezungumzia hii press nikiwa na uhakika lakini kuna watu wachache ambao sijui nia yao ni nini?, tukijaribu kufanya wao wanatufundisha, kikundi hiki cha watu wachache ambao ndio wamejenga imani ya kutoliamini jeshi la polisi, wao…

Soma Zaidi >>

DC KATAMBI NA MBUNGE MAVUNDE WASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WAENDESHA BAJAJI NA BODABODA JIJI LA DODOMA.

  Dodoma Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mheshimiwa Patrobas Katambi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mheshimiwa Anthony Mavunde jana tarehe 19/10/2018 wamesikiliza na kutatua kero za maelfu ya waendesha bajaji na bodaboda wanaofanya shughuli zao katika Jiji la Dodoma. Viongozi hao wameahidi kuwa bega kwa bega na waendesha bajaj na bodaboda kwa kuwataka kuanzisha Umoja wenye nguvu ili waweze kuwawezesha kupitia fursa mbalimbali za mikopo,huku DC Katambi akisisitiza utii wa sheria bila shurti na kulitaka Jeshi la Polisi kuanzisha dawati maalum la kushughulikia matatizo ya waendesha…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI “WANANGU NENDENI MKASHINDE, NENDENI MKAPEPERUSHE VIZURI BENDERA YA TANZANIA, LENGO LETU IWE NI KUSHINDA TU”

Ikulu Dar es salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) kuongeza juhudi za kupata ushindi katika michuano mbalimbali inayoshiriki ikiwemo ya kufuzu fainali za michuano ya Afrika (AFCON) itakayofanyika mwakani nchini Cameroon. Mhe. Rais Magufuli amesema hayo alipokutana na kuzungumza na wachezaji wa Taifa Stars na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Magufuli ambaye amechangia Taifa Stars shilingi Milioni…

Soma Zaidi >>