ZITTO: KWANINI SERIKALI INAOGOPA WACHUNGUZI WA KIMATAIFA? USHAURI WA LEMA NI MZURI.

  Jana Jumanne, siku ya 6 tangu Mohammed Dewji, mfanyabiashara na mlezi wa Klabu ya Simba atekwe nyara, Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani Bwana Godbless Lema alitoa pendekezo kuwa Serikali ya Tanzania iombe msaada wa nje kuongeza juhudi za kumtafuta na kumwokoa Mohammed, Jana hiyo hiyo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Masauni alijibu kuwa Serikali haitafanya hivyo kwa sababu jeshi la polisi nchini lina uwezo na utaalamu wa kutosha kuendelea na uchunguzi. Naibu Waziri hayupo sahihi kukataa pendekezo la Waziri Kivuli nashauri kuwa pendekezo la Waziri Kivuli…

Soma Zaidi >>

KESI YA TIDO MHANDO YAENDELEA KUSOTA MAHAKAMANI

    Dar Es Salaam Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando ameshindwa kuulizwa maswali na upande wa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai kushindwa kufika Mahakamani. Naye Wakili wa upande wa Serikali alitoa Sababu zilizomfanya Hakimu kushindwa kufika Mahakamani hapo akisema Hakimu ameshindwa kufika mahakamani kwa Sababu amesafiri kuelekea Msoma, hivyo yupo safarini Musoma mkoani Mara kwa shughuli nyingine za kiofisi. Wakili wa TAKUKIRU,Bwana Dismas Muganyizi, alieleza mahakamani mbele…

Soma Zaidi >>

WATU 16 WANAODAIWA KUWA NI WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA ILALA

  Naibu Kamishna uhamiaji, Afisa uhamiaji Ilala Pili Zuberi Mdanku kwa kushirikiana na OCD Ilala SP Jason Ibrahim wamefanikiwa kuwakamata watu 16 wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu katika kata ya Mchikichini Jimbo la ilala. Hatua hiyo, imekuja mara baada ya mmoja wa wananchi kutoa kero kwa mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuwa kuna nyumba ambayo inawahifadhi wahamiaji haramu. DCI Pili ameamua kufanya doria katika eneo hilo mara baada ya kupata taarifa hizo kwani, si mara ya kwanza kufanya doria katika eneo hilo na kuwakamata wahamiaji haramu. Amesema kuwa,…

Soma Zaidi >>

PROF MAKAME MBARAWA AHIMIZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI

    Dar Es Salaam. Waziri wa Maji, Mheshimiwa Makame Mbarawa amewaasa wananchi wote wanaovizunguka vyanzo vya maji kuvilinda na kuvitunza kwa manufaa yao na taifa. Profesa Mbarawa ametoa rai hiyo akiwa kwenye chanzo cha maji cha Mtoni, kilichopo Wilaya ya Temeke na kuonya kuhusu uharibifu wa vyanzo unavyoweza kusababisha athari za upungufu wa maji ya uhakika kwa miaka ijayo. ”Rai yangu kwa wanaoishi eneo la chanzo hiki cha Mtoni ambacho kinazalisha lita milioni 9 kwa siku, kikiwa moja ya vyanzo vitatu vinavyotumiwa na mkoa wa Dar es Salaam ni…

Soma Zaidi >>

KANISA KATOLIKI KUADHIMISHA KILELE CHA MIAKA 150 YA UINJILISHAJI BAGAMOYO.

    Dar Es Salaam Na Augustine Richard Darmpya.com Askofu Mkuu wa jimbo kuu la Dar Es Salaam Kardinali Mwadhama Polycarp Pengo leo tarehe 17/10/2018 amezungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kuelezea kilele cha miaka 150 ya uinjilishaji katika Kanisa katoliki akisema “Kanisa Katoliki limekuwepo katika nchi yetu kwa zaidi ya Miaka 150 iliyopita ambapo kwa hapa Tanzania bara wamisionari ambao ndiyo walikuwa waenezaji wakuu wa dini ya kikatoliki walifikia Bagamoyo ambapo ndipo tutakapoazimisha Miaka 150 ya uijilishaji Mwaka huu. “Tofauti ya Wamisionari na walikuwa wanafanya biashara…

Soma Zaidi >>

RC KATAVI AMTAKA MKANDARASI KUONGEZA KASI UJENZI WA JENGO LA UTAWALA NA NYUMBA ZA WATUMISHI HALMASHAURI YA MPANDA

  Katavi, Mkuu wa Mkoa wa Katavi ya mheshimiwa Amos Makala jana tarehe 16/10/2018 amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali iliyopo mkoani katavi. Akiwa wilaya ya Tanganyika halmashauri ya Mpanda Mkuu wa mkoa alimuasa Mkandarasi kutoka SUMA JKT aliyepewa tenda ya ujenzi wa nyumba za watumishi pamoja na jengo la Utawala kuongeza jitihada katika ujenzi wa majengo hayo ili yaweze kukamilika kabla ya January 2019 ili yaaanze kutumika mara moja . Aidha amewataka vijana wanaopata nafasi za ajira katika Kampuni za ujenzi wa Barabara mkoani Katavi kuacha tabia ya…

Soma Zaidi >>

NAIBU SPIKA AFANIKISHA ZAIDI YA SH MILION 15 KWA AJILI YA BWENI.

  Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amefanikisha kupatikana zaidi ya shilingi milioni 15 katika harambee ya kuchangia shule ya sekondari ya wasichana Archbishop Mayala . Shule ya hiyo ya wasichana iliyopo kijiji cha Ibindo Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wanafunzi 55 ambapo kwa sasa mwaka 2018 shule ina wanafunzi 519. Katika harambee hiyo marafiki wa Dkt. Tulia mkoa wa Simiyu wamechangia sh.300,000/= pamoja na miche ya maparachichi 40 kwa ajili kupanda kwenye shamba la shule hiyo. Bweni hilo…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI WA TUME YA MAREKEBISHO YA SHERIA NCHINI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. January Henry Msofe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria. Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewateua Bw. Iddi Mandi na Bw. Julius Kalolo Bundala kuwa Makamishna wa muda wa Tume ya Kurekebisha Sheria. Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Paul Kimiti kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ranchi za Taifa (NARCO). Uteuzi wa viongozi hao umeanza tarehe 14 Oktoba, 2018.  

Soma Zaidi >>