Serikali kuwashughulikia wazazi ambao watoto wao watakeketwa

Ni msimu wa ukeketaji kwa wasichana na Tohara kwa Wavulana ukiwa umeanza wilayani Tarime, Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema itawakamata na Kuwafikisha mahakamani Wazazi ambao watoto wao wakike watakeketwa. Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii  kitengo cha malezi na Familia,Grace Mwangwa alipokuwa akitoa tamko la Serikali kwenye mkutano wa kujadili namna ya kukomesha ukeketaji ulioandaliwa na shirika la Utu wa Mtoto CDF uliofanyika ukumbi wa Blue Sky mjini Tarime. Mwangwa anasema kuwa kitendo cha kuwakamata Mangariba pekee hakiwezi…

Soma Zaidi >>

MWAKYEMBE MGENI RASMI TAMASHA LA TaSUBa.

  Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 20 katika taasisi hiyo iliyopo Mjini Bagamoyo, Mkoani Pwani. Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Oktoba 15,2018, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dk Herbert Makoye amebainisha kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku akiwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo. Aidha amesema, katika ufungaji wa tamasha hilo, mgeni rsmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari…

Soma Zaidi >>

BASI LA NEW FORCE LATUMBUKIA MLIMA KITONGA.

    Watu kadhaa wamenusurika kifo katika ajali iliyotokea hii leo katika mteremko wa Mlima Kitonga mkoani Iringa baada ya basi la kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es salaaam kugongana na gari nyingine linalodaiwa kuwa ni la kampuni ya Golden deer lilikuwa likitokea Dar kwenda Tunduma na kisha kuanguka chini ya mlima huo wenye mteremko mkali. Kaimu kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa , Deusdedit Kashindo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa taarifa za awali zinasema kuna majeruhi tu.

Soma Zaidi >>

VIKAO VYA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE KUANZA KUUNGURUMA BUNGENI.

  DODOMA  TANZANIA Vikao vya Kamati 14 za Kudumu za Bunge vitaanza Jumatatu tarehe 22Oktoba na kuendelea hadi tarehe 04 Novemba 2018,Jijini Dodoma. Shughuli zote za Kamati katika kipindi hicho zimepangwa kwa kuzingatia Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016. Shughuli hizo ni kama ifuatavyo; Moja ni Uchambuzi wa Taarifa mbalimbali za Msajili wa Hazina kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma katika Mashirika naTaasisi mbalimbali Nchini. Mbili Uchambuzi waTaarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu za Mwaka 2016/2017 Tatu,…

Soma Zaidi >>

DC MJEMA AWATAKA VIONGOZI KUWAJIBIKA

    Dar es Salaam Mkuu wa wilaya ya Ilala, mheshimiwa Sophia Mjema amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mtaa hadi Wilaya kuwajibika kwa kuwahudumia kwa kuwasikiliza kero zao na kuzitatua. Kauli hiyo ameitoa mapema leo wakati alipokua katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika jimbo la Ilala kata ya Mchafukoge na Kisutu. Amesema kuwa, amekuwa akipokea kero mbalimbali kwa wananchi na kuzitatua, ambapo amebaini viongozi wanaenda kukaa ofisini na kuondoka hawawafikii wa kuwasikiliza kero zao. “Viongozi wote naomba tuwajibike kuanzia ngazi ya mtaa hadi wilaya ili…

Soma Zaidi >>

TANZANIA INAVYONUFAIKA NA MFUKO WA MAZIGIRA WA DUNIA

  Mfuko wa Mazingira Duniani (Global Environment Facility –GEF) ulianzishwa mwaka 1991. Lengo la Mfuko huu ni kutoa fedha kwa nchi zinazoendelea na zinazoinukia kiuchumi, ambazo ni wanachama wa mikataba mabalimbali ya kimataifa ya mazingira kwa ajili ya kugharamia shughuli/miradi mbalimbali ya kukabiliana na changamoto sita za mazingira ambazo zimeonekana kuwa ni tishio kwa Dunia. Changamoto hizo ni (1) Kupotea kwa Bioanuai Duniani (Loss of Biodiversity); (2) Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Change); (3) Uharibifu wa Ardhi (Land degradation); (4) Uchafuzi wa Maji ya Kimataifa (International Waters’ Pollution); (5) Kumong’onyoka kwa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MWAKYEMBE MGENI RASMI TAMASHA LA KIMATAIFA LA BAGAMOYO

Waziri  wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi  wa Tamasha la 37 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo litakalofanyika Oktoba 20 katika taasisi hiyo iliyopo Mjini Bagamoyo, Mkoani Pwani. Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Oktoba 15,2018,  Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dk Herbert Makoye amebainisha kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku akiwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo. Dkt. Makoye amsema katika ufungaji wa tamasha hilo, mgeni rsmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Habari…

Soma Zaidi >>

SERIKALI KUPAMBANA NA UCHOMAJI HOLELA WA TAKA

  Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na UNIDO jana tarehe 15/10/2018 wamezindua warsha ya Mradi wa kudhibiti kemikali zitokanazo na uchomaji wa taka katika maeneo ya wazi. Akizindua warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine amesema kuwa mradi huo unatarajia kuja na mapendekezo ya namna ya kupunguza athari za uchomaji taka katika mazingira. Balozi Sokoine amesema kuwa lengo kubwa la warsha hiyo ya wataalamu ni kujadili mbinu bora za uchomaji taka bila kuathiri…

Soma Zaidi >>

BABA ALIYE MBAKA MWANAE AFIKISHWA MAHAKAMANI.

  Mpwapwa -Dodoma Katika kesi ya ubakaji namba 41 ya mwaka 2018 inayo mkabili mtuhumiwa Jemsi Leuna kwa tuhuma za kumbaka mwanae wa miaka 12 imeendelea leo tarehe 16/10/2018 katika Mahakama ya wilaya Mpwapwa. Kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu mkazi mfawidhi Nurupedesia Nassary. Katika kesi hiyo Mtuhumiwa anayetuhumiwa kwa kumbaka mtoto wake wa Kike kinyume na kifungu cha sheria cha 158 kifungu kidogo cha 1(a) cha Kanuni ya adhabu namba 16 iliyo fanyiwa marekebisho  mwaka 2002. Aidha kosa la pili linalo mkabili Mtuhumiwa ni kumpa ujauzito  mwanae huyo ambae ni…

Soma Zaidi >>

WANANCHI WALIOPISHA MRADI WA UMEME WA KV400 KUTOKA SINGIDA HADI NAMANGA WAANZA KULIPWA FIDIA.

    Serikali imeanza kulipa fidia kwa Wananchi 4000 waliopisha mradi wa kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa Kilovolti 400 kutoka Singida hadi Namanga ambapo zoezi la ulipaji fidia litakamilika hivi karibuni. Mradi huo wa kusafirisha Umeme wa KV400 kutoka Singida hadi Namanga utaunganisha nchi za Tanzania na Kenya na unafahamika kama Kenya – Tanzania Power Interconnector Project(KTPIP). Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu alisema hayo alipotembelea eneo la kuhifadhia vifaa vya mradi huo (yard) katika kijiji cha Nangwa wilayani Hanang mkoani Manyara, mwishoni mwa wiki, ili kukagua vifaa hivyo…

Soma Zaidi >>