MH MABULA AENDELEA NA ZIARA YA MTAA KWA MTAA KUSIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Nyamagana, MWANZA. Mbunge Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Mheshimiwa Stanislaus Mabula, kabla na baada ya ziara zake za mrejesho wa bunge la bajeti kwa wananchi kila kata, sasa ameanza ziara ya mtaa kwa mtaa katika mitaa yote yenye changamoto za muda mrefu na za muda mfupi. Haya yamebainishwa leo Septemba 25, 2018 na Mh Mabula alipowatembelea wananchi wa mtaa wa Nyamayuki kata ya Mahina, kusikiliza malalamiko yaliyowasilishwa kwake kupitia mikutano ya hadhara sanjari na maombi kupitia Ofisi yake. Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula akijibu baadhi ya hoja wakati…

Soma Zaidi >>

CHADEMA WAZINDUA SERA MPYA ILIYO NA MAENEO MAKUU MATATU

Na John Marwa@Darmpya.com Dar es Salaam. Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezidua sera mpya ya mwaka 2018 iliyogawanyika kwenye maeneo matatu. Akizungumza na viongozi na wanachama kutoka maeneo mbalimbali ya nchi waliohudhuria uzinduzi huo leo Septemba 25, 2018, Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Aikael Mbowe, amesema sera hizo zitakuwa zinafanyiwa marekebisho kulingana na wakati. Mbowe ambaye ni mbunge jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, amesema eneo la kwanza lililoko kwenye sera hiyo ni ile inayolinda uhuru wa wananchi, huku akielezea kuwa Mwl Julius Nyerere aliwahi…

Soma Zaidi >>

NIGERIA YAENDELEA KUWATAFUTA MABAHARIA 12 WALIOTEKWA NA MAHARAMIA

Lagos, NIGERIA. Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa inafanya kila iliwezalo ili kuwapata mabaharia 12, nahodha, msaidizi wake, mafundi na wafanyakazi wengine wa meli ya mizigo waliotekwa nyara na maharamia mwishoni mwa juma lililopita katika pwani ya Delta nchini Niger. Mamlaka ya utawala na Udhibiti wa Usafiri wa majini nchini Nigeria (NIMASA) imetangaza kwamba imeanza zoezi la utafutaji na uokoaji kwa wafanyakazi wa Glarus, meli ya kampuni ya Uswisi ya Massoel Shipping. Mkurugenzi Mkuu wa NIMASA, Dakuku Peterside, amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Lagos kuwa, Mamlaka yake inafanya…

Soma Zaidi >>

WATU ISHIRINI NA MOJA WAJERUHIWA KATIKA MAKABILIANO HUKO NCHINI KENYA

Narok, KENYA. Watu wapatao ishirini na moja (21) wamejeruhiwa baada ya kuzuka tena kwa mapigano kati ya jamii mbili zinazoishi katika kaunti ya Narok nchini Kenya. Mwakilishi wa serikali katika eneo hilo, George Natembeya, amesema, mapigano hayo yalizuka siku ya Jumapili baada ya familia moja kuibiwa mifugo yake. “Waliojeruhiwa walichomwa na mishale, na wamepelekwa hospitali kupata matibabu. Waathirika wanne wamekubaliwa kwenye Hospitali ya Tenwek Mission huko Bomet County.” Amesema Natembeye. Aidha, jeshi la polisi nchini humo limetuma maofisa wa usalama eneo hilo baada ya tukio hilo ili kuwasaka wahusika. Makabiliano…

Soma Zaidi >>

UNICEF:WATOTO NUSU MILIONI NCHINI LIBYA WAKO KATIKA HATARI

Shirika la Umoja wa Mataifa kwa Watoto (UNICEF), limesema takriban watoto laki tano (500,00) nchini Libya wako katika hatari katika mji wa Tripoli, ambao unakabiliwa na makabiliano mabaya kwa mwezi mmoja sasa. Kuanzia tarehe 27 Agosti, mapigano kati yamakundi hasimu yameuwa watu zaidi ya 115 na karibu 400 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa ripoti ya mwisho ya wizara ya afya iliyochapishwa juzi usiku siku ya Jumamosi. “Mapigano yameongezeka ndani ya saa 48 Kusini mwa Tripoli na watoto zaidi ya nusu milioni wako katika hatari katika mji mkuu wa Libya , Unicef…

Soma Zaidi >>

SANAMU YA NELSON MANDELA YAZINDULIWA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA

New York, MAREKANI. Sanamu ya aliyekuwa Rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini,Marehemu Nelson Mandela, imezinduliwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York nchini Marekani. Hii ndio sanamu pekee katika Makao makuu ya Umoja huo na inaashiria juhudi za Mandela za kuliunganisha dunia na kuhimiza amani wakati alipokuwa hai. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, amezindua sanamu hiyo ya kihistoria na kusema inaeleza mchango wa Afrika Kusini katika amani ya dunia. Sanamu kubwa zaidi duniani ya Nelson Mandela iliwahi kuzinduliwa katika mji mkuu wa Afrika kusini Pretoria…

Soma Zaidi >>

MTOTO WA RAIS MSTAAFU ANGOLA DOS SANTOS AZUILIWA KUTOKANA NA RUSHWA.

  Luanda, ANGOLA. Mtoto wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, Jose Filomeno Dos Santos, amezuiwa kwa muda kutokana na kesi ya rushwa ya Dola milioni 500, ambapo Hakimu Mkuu wa Jamhuri amesema kuzuiliwa kwake ni kutokana na ugumu wa kesi. Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu nchini Angola, uchunguzi umeanza na kwamba kuzuiliwa kwa Jose Filomeno Dos Santos ni kutokana na ugumu wa kesi lakini pia ni kutaka kuweka wazi kesi hii kuhakikisha pia ufanisi katika uchunguzi. Mwanasheria huyo amesema kuna ushahidi tosha unaothibitisha kuwa watuhumiwa walijihusisha…

Soma Zaidi >>

KATIBU MKUU UN KUHUTUBIA LEO BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA.

  New York, MAREKANI. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anatarajiwa kuelezea hali halisi ya ulimwengu hivi sasa wakati atakapohutubia mkutano wa kila mwaka wa  baraza kuu la Umoja wa Mataifa. Akizungumzia kwa ufupi juu ya hotuba hiyo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema Guterres pia atazungumzia kuhusu masuala  yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kusisitiza kuwa watu wote lazima wanufaike na tekinolojia mpya. Aidha atatoa mwito kwa viongozi wa kidunia juu ya haja ya kushikamana  kwa ajili…

Soma Zaidi >>

WATU 21 WAUAWA HUKO BENI JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

Kinshasa, DRC. Jeshi la Ulinzi na Usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), limetoa ripoti mpya ya watu 21 waliouawa na limesema limeanzisha uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea huko Beni, mashariki mwa nchi hiyo. Mauaji hayo yamehusishwa kundi la kigaidi la waasi wa Uganda la Allied Democratic Force (ADF). “Ofisi ya mashitaka ya kijeshi imefungua uchunguzi kuhusu mashambulizi mabaya yaliyoendeshwa na kundi la Kiislamu la ADF Beni dhidi ya wakaazi wa Beni, na kusababisha vifo vya raia 17 na wanajeshi 4,” amesema Kanali Khumbu Ngoma afisa wa mashitaka katika mkoa…

Soma Zaidi >>

DC MJEMA AWATAKA VIONGOZI WA KATA NA MITAA KUWAJIBIKA

Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema mpaka sasa amekusanya kero 135 katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua katika jimbo la Segerea na Ukonga. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema leo baada ya kuskiliza kero za wananchi katika kata ya tabata amesema kuwa, kero hizo zimechangiwa na viongozi wa mitaa na kata kutokuwajibika vizur. “Changamoto zote nilizokutana ni wazi kuwa viongozi wa mtaa na kata hawawafikii wananchi kuwasikiliza kero zao na kuweza kuzitatua, hivyo kupelekea mrundikano wa kero”…

Soma Zaidi >>