VIDEO : RAIS MAGUFULI AMUONYA RC MAKONDA NA KUMTAKA ALIPIE KODI MAKONTENA YAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka viongozi wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria sambamba na kuhakikisha wanasimamia ipasavyo matumizi ya rasilimali za umma kwa maslahi ya wananchi. Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo tarehe 30 Agosti, 2018 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita, wakati akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa wilaya hiyo, ambapo amesisitiza kuwa viongozi wote wajenge utaratibu wa kusoma sheria na kujiepusha kutumiwa kwa maslahi ya watu binafsi. Huku akitolea mfano wa mgogoro wa makontena…

Soma Zaidi >>

MAKONDA : WAZAZI WARUHUSUNI WATOTO KUPATA CHANJO MASHULENI

Na Heri Shaban Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda amezindua kampeni ya uhamasishaji wa utoaji dawa kinga tiba za kichocho na minyoo kwa wanafunzi wa shule za msingi 678,189 ambao wanatarajia kupatiwa chanjo hiyo katika mkoa huo. Akizindua kampeni hiyo Makonda amesema chanjo hiyo itatolewa katika shule 708 za msingi zilizopo katika manispaa za mkoa mzima. “Nawaomba wazazi muwaruhusu watoto wetu wa shule za msingi katika kuwapatia chanjo hii kwani chanjo ni bora kuliko tiba elimu ishatolewa kwa walimu wa shule zote za serikali na binafsi” – Amesema…

Soma Zaidi >>

DC SOPHIA KIZIGO AWAVAA WANAFUNZI NA KUWATAKA KUTOKUWA UCHAFU

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Mh Sophia Kizigo amewataka wanafunzi wilayani humo kuzingatia masomo na kuacha kufanya mambo machafu yasiyohusiana na taaluma zao ili waweze kufikia malengo yao na kufanikiwa katika maisha kwa ujumla. Amesema hayo alipotembelea shule ya sekondari ya Nasuli ambayo ilikuwa ya kwanza kwa mkoa huo na kuwataka wanafunzi shuleni humo kuwa na nidhamu kwenye masomo yao baada ya hapo awali kufanya vizuri kimkoa na anatarajia matokeo mazuri zaidi kitaifa kupitia shule hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mhe. Sophia Kizigo akipokea taarifa kutoka kwa…

Soma Zaidi >>

ZAIDI YA WANAFUNZI LAKI MBILI KUPATA CHANJO YA MINYOO NA KICHOCHO, ILALA

Na Heri Shaban Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam imeanza kampeni ya utoaji chanjo ya magonjwa yaliokuwa hayapewi kipaumbele kwa shule zake za Msingi zote za serikali pamoja na binafsi lengo la kutoa chanjo hiyo kuzuia watoto hasa wanafunzi wasipatwe na magonjwa hayo kutokana na kutumia maji ya katika madimbwi na mabwawa. Mganga mkuu wa Manispaa ya Ilala Dkt Emily Lihawa (Picha na Heri Shaban). Akingumza Dar es salaam leo mganga mkuu wa manispaa Ilala Dkt Emily Lihawa katika uzinduzi wa kampeni hiyo wilaya ya Ilala katika kikao cha…

Soma Zaidi >>

WAZAZI NA WALEZI SERENGETI WATAKIWA KUWA NA MGAWANYO SAWA WA MAJUKUMU YA KAZI KWA WATOTO WAO.

Wazazi na walezi wilayani Serengeti mkoani Mara wametakiwa kuachana na suala la ubaguzi katika mgawanyo wa majukumu  ya kazi  majumbani ili kuleta usawa wa kijinsia  huku mtoto wa kike akilimbikiziwa kazi nyingi kuliko mtoto wa kiume majumbani. Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi wakiimba  Shairi lenye ujumbe wa kupiga vita Ukatili. Hayo yamebainishwa na wanafunzi katika tamasha la kutoa elimu juu ya masuala ya kupinga mila na desturi zilizopitwa na wakati zikiwemo ukeketaji, ndoa za utotoni pamoja na mimba za utotoni, tamasha lililoandaliwa na shirika la RIGTH TO PLAY na…

Soma Zaidi >>